Translations | Suras |
KISWAHILI | |
80 - A'BASA | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
1 | Alikunja kipaji na akageuka, |
2 | Kwa sababu alimjia kipofu! |
3 | Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika? |
4 | Au atawaidhika, na mawaidha yamfae? |
5 | Ama ajionaye hana haja, |
6 | Wewe ndio unamshughulikia? |
7 | Na si juu yako kama hakutakasika. |
8 | Ama anaye kujia kwa juhudi, |
9 | Naye anaogopa, |
10 | Ndio wewe unampuuza? |
11 | Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana. |
12 | Basi anaye penda akumbuke. |
13 | Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa, |
14 | Zilizo inuliwa, zilizo takaswa. |
15 | Zimo mikononi mwa Malaika waandishi, |
16 | Watukufu, wema. |
17 | Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha? |
18 | Kwa kitu gani amemuumba? |
19 | Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria. |
20 | Kisha akamsahilishia njia. |
21 | Kisha akamfisha, akamtia kaburini. |
22 | Kisha apendapo atamfufua. |
23 | La! Hajamaliza aliyo muamuru. |
24 | Hebu mtu na atazame chakula chake. |
25 | Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu, |
26 | Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu, |
27 | Kisha tukaotesha humo nafaka, |
28 | Na zabibu, na mimea ya majani, |
29 | Na mizaituni, na mitende, |
30 | Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara, |
31 | Na matunda, na malisho ya wanyama; |
32 | Kwa manufaa yenu na mifugo yenu. |
33 | Basi utakapo kuja ukelele, |
34 | Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye, |
35 | Na mamaye na babaye, |
36 | Na mkewe na wanawe - |
37 | Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha. |
38 | Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri, |
39 | Zitacheka, zitachangamka; |
40 | Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi, |
41 | Giza totoro litazifunika, |
42 | Hao ndio makafiri watenda maovu. |
ReadTheQuran.org |