Translations | Suras |
KISWAHILI | |
83 - AL - MUT'AFFIFIIN | |
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. | |
1 | Ole wao hao wapunjao! |
2 | Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe. |
3 | Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza. |
4 | Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa |
5 | Katika Siku iliyo kuu, |
6 | Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote? |
7 | Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin. |
8 | Unajua nini Sijjin? |
9 | Kitabu kilicho andikwa. |
10 | Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha! |
11 | Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo. |
12 | Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi. |
13 | Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale! |
14 | Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma. |
15 | Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi. |
16 | Kisha wataingia Motoni! |
17 | Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha. |
18 | Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin. |
19 | Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin? |
20 | Kitabu kilicho andikwa. |
21 | Wanakishuhudia walio karibishwa. |
22 | Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema. |
23 | Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia. |
24 | Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema, |
25 | Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri, |
26 | Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana. |
27 | Na mchanganyiko wake ni Tasniim, |
28 | Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa. |
29 | Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini. |
30 | Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana. |
31 | Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi. |
32 | Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea. |
33 | Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao. |
34 | Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri, |
35 | Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia. |
36 | Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda? |
ReadTheQuran.org |