68 - AL - QALAM |
| |
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
| |
| |
| 1 | Nuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo, |
| |
| 2 | Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu. |
| |
| 3 | Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika. |
| |
| 4 | Na hakika wewe una tabia tukufu. |
| |
| 5 | Karibu utaona, na wao wataona, |
| |
| 6 | Ni nani kati yenu aliye pandwa na wazimu. |
| |
| 7 | Hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye ajuaye zaidi nani aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka. |
| |
| 8 | Basi usiwat'ii wanao kadhibisha. |
| |
| 9 | Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie. |
| |
| 10 | Wala usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa, |
| |
| 11 | Mtapitapi, apitaye akifitini, |
| |
| 12 | Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi, |
| |
| 13 | Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu. |
| |
| 14 | Ati kwa kuwa ana mali na watoto! |
| |
| 15 | Anapo somewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za uwongo za watu wa zamani! |
| |
| 16 | Tutamtia kovu juu ya pua yake. |
| |
| 17 | Hakika tumewajaribu hawa kama tulivyo wajaribu wale wenye shamba, walipo apa kwamba watayavuna mazao yake itakapo kuwa asubuhi. |
| |
| 18 | Wala hawakusema: Mungu akipenda! |
| |
| 19 | Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako Mlezi, nao wamelala! |
| |
| 20 | Likawa kama usiku wa giza. |
| |
| 21 | Asubuhi wakaitana. |
| |
| 22 | Ya kwamba nendeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna. |
| |
| 23 | Basi walikwenda na huku wakinong'onezana, |
| |
| 24 | Ya kuwa leo hata masikini mmoja asikuingilieni. |
| |
| 25 | Na walikwenda asubuhi, nao wameshikilia azimio hilo. |
| |
| 26 | Basi walipo liona, wakasema: Hakika tumepotea! |
| |
| 27 | Bali tumenyimwa! |
| |
| 28 | Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu? |
| |
| 29 | Wakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu. |
| |
| 30 | Basi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao. |
| |
| 31 | Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka! |
| |
| 32 | Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. |
| |
| 33 | Namna hivi yanakuwa mateso, na bila ya shaka mateso ya Akhera ni makubwa zaidi, laiti wangeli jua! |
| |
| 34 | Hakika wachamngu watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao Mlezi. |
| |
| 35 | Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu? |
| |
| 36 | Mna nini? Mnahukumu vipi? |
| |
| 37 | Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma? |
| |
| 38 | Kuwa mtapata humo mnayo yapenda? |
| |
| 39 | Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika mtapata kila mnayo jihukumia? |
| |
| 40 | Waulize: Ni nani miongoni mwao dhamini wa haya? |
| |
| 41 | Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanasema kweli. |
| |
| 42 | Siku utakapo wekwa wazi mundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza, |
| |
| 43 | Macho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipo kuwa wazima - |
| |
| 44 | Basi niache na wanao kadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kwa mahali wasipo pajua. |
| |
| 45 | Na ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni imara. |
| |
| 46 | Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo? |
| |
| 47 | Au iko kwao siri, basi wao wanaiandika? |
| |
| 48 | Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe kama mmezwa na samaki, alipo nadi naye kazongwa. |
| |
| 49 | Kama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa. |
| |
| 50 | Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema. |
| |
| 51 | Na walio kufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanapo sikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu. |
| |
| 52 | Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. |
| |