69 - AL - H'AAQQAH |
| |
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
| |
| |
| 1 | Tukio la haki. |
| |
| 2 | Nini hilo Tukio la haki? |
| |
| 3 | Na nini kitakujuulisha nini hilo Tukio la haki? |
| |
| 4 | Thamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unao situsha. |
| |
| 5 | Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno. |
| |
| 6 | Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usio zuilika. |
| |
| 7 | Alio wapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani. |
| |
| 8 | Basi je! Unamwona mmoja wao aliye baki? |
| |
| 9 | Na Firauni na walio mtangulia, na miji iliyo pinduliwa chini juu, walileta khatia. |
| |
| 10 | Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu. |
| |
| 11 | Maji yalipo furika Sisi tulikupandisheni katika safina, |
| |
| 12 | Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalo sikia liyahifadhi. |
| |
| 13 | Na litapo pulizwa barugumu mpulizo mmoja tu, |
| |
| 14 | Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja, |
| |
| 15 | Siku hiyo ndio Tukio litatukia. |
| |
| 16 | Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa. |
| |
| 17 | Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi. |
| |
| 18 | Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu. |
| |
| 19 | Basi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu! |
| |
| 20 | Hakika nalijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu. |
| |
| 21 | Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza, |
| |
| 22 | Katika Bustani ya juu, |
| |
| 23 | Matunda yake yakaribu. |
| |
| 24 | Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita. |
| |
| 25 | Na ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu! |
| |
| 26 | Wala nisingeli jua nini hisabu yangu. |
| |
| 27 | Laiti mauti ndiyo yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa. |
| |
| 28 | Mali yangu hayakunifaa kitu. |
| |
| 29 | Madaraka yangu yamenipotea. |
| |
| 30 | (Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu! |
| |
| 31 | Kisha mtupeni Motoni! |
| |
| 32 | Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini! |
| |
| 33 | Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, |
| |
| 34 | Wala hahimizi kulisha masikini. |
| |
| 35 | Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu, |
| |
| 36 | Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni. |
| |
| 37 | Chakula hicho hawakili ila wakosefu. |
| |
| 38 | Basi naapa kwa mnavyo viona, |
| |
| 39 | Na msivyo viona, |
| |
| 40 | Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima. |
| |
| 41 | Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini. |
| |
| 42 | Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka. |
| |
| 43 | Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
| |
| 44 | Na lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu, |
| |
| 45 | Bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia, |
| |
| 46 | Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo! |
| |
| 47 | Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeli weza kutuzuia. |
| |
| 48 | Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wachamngu. |
| |
| 49 | Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha. |
| |
| 50 | Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanao kataa. |
| |
| 51 | Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini. |
| |
| 52 | Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu. |
| |