75 - AL - QIYAMAH |
| |
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
| |
| |
| 1 | Ninaapa kwa Siku ya Kiyama! |
| |
| 2 | Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu! |
| |
| 3 | Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake? |
| |
| 4 | Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake! |
| |
| 5 | Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake. |
| |
| 6 | Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama? |
| |
| 7 | Basi jicho litapo dawaa, |
| |
| 8 | Na mwezi utapo patwa, |
| |
| 9 | Na likakusanywa jua na mwezi, |
| |
| 10 | Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio? |
| |
| 11 | La! Hapana pa kukimbilia! |
| |
| 12 | Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu. |
| |
| 13 | Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha. |
| |
| 14 | Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake. |
| |
| 15 | Na ingawa atatoa chungu ya udhuru. |
| |
| 16 | Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka. |
| |
| 17 | Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha. |
| |
| 18 | Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake. |
| |
| 19 | Kisha ni juu yetu kuubainisha. |
| |
| 20 | Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani, |
| |
| 21 | Na mnaacha maisha ya Akhera. |
| |
| 22 | Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara, |
| |
| 23 | Zinamwangallia Mola wao Mlezi. |
| |
| 24 | Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana. |
| |
| 25 | Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo. |
| |
| 26 | La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo, |
| |
| 27 | Na pakasemwa: Nani wa kumganga? |
| |
| 28 | Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki; |
| |
| 29 | Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi, |
| |
| 30 | Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi! |
| |
| 31 | Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali. |
| |
| 32 | Bali alikanusha, na akageuka. |
| |
| 33 | Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao. |
| |
| 34 | Ole wako, ole wako! |
| |
| 35 | Kisha Ole wako, ole wako! |
| |
| 36 | Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure? |
| |
| 37 | Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa? |
| |
| 38 | Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo. |
| |
| 39 | Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke. |
| |
| 40 | Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu? |
| |