79 - ANNAZIA'AT |
| |
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
| |
| |
| 1 | Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu, |
| |
| 2 | Na kwa wanao toa kwa upole, |
| |
| 3 | Na wanao ogelea, |
| |
| 4 | Wakishindana mbio, |
| |
| 5 | Wakidabiri mambo. |
| |
| 6 | Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka, |
| |
| 7 | Kifuate cha kufuatia. |
| |
| 8 | Siku hiyo nyoyo zitapiga piga, |
| |
| 9 | Macho yatainama chini. |
| |
| 10 | Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza? |
| |
| 11 | Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa? |
| |
| 12 | Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara! |
| |
| 13 | Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu, |
| |
| 14 | Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano! |
| |
| 15 | Je! Imekufikia hadithi ya Musa? |
| |
| 16 | Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la T'uwaa, akamwambia: |
| |
| 17 | Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri. |
| |
| 18 | Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa? |
| |
| 19 | Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha. |
| |
| 20 | Basi alimwonyesha Ishara kubwa. |
| |
| 21 | Lakini aliikadhibisha na akaasi. |
| |
| 22 | Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi. |
| |
| 23 | Akakusanya watu akanadi. |
| |
| 24 | Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa. |
| |
| 25 | Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo. |
| |
| 26 | Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa. |
| |
| 27 | Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga! |
| |
| 28 | Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri. |
| |
| 29 | Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake. |
| |
| 30 | Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi. |
| |
| 31 | Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake, |
| |
| 32 | Na milima akaisimamisha, |
| |
| 33 | Kwa nafuu yenu na mifugo yenu. |
| |
| 34 | Basi itakapo fika hiyo balaa kubwa, |
| |
| 35 | Siku ambayo mtu atakumbuka aliyo yafanya, |
| |
| 36 | Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona, |
| |
| 37 | Basi ama yule aliye zidi ujeuri, |
| |
| 38 | Na akakhiari maisha ya dunia, |
| |
| 39 | Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake! |
| |
| 40 | Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio, |
| |
| 41 | Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake! |
| |
| 42 | Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini? |
| |
| 43 | Una nini wewe hata uitaje? |
| |
| 44 | Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake. |
| |
| 45 | Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuikhofu. |
| |
| 46 | Ni kama kwamba wao siku watapo iona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake. |
| |