100 - AL - A'ADIYAAT |
| |
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
| |
| |
| 1 | Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua, |
| |
| 2 | Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini, |
| |
| 3 | Wakishambulia wakati wa asubuhi, |
| |
| 4 | Huku wakitimua vumbi, |
| |
| 5 | Na wakijitoma kati ya kundi, |
| |
| 6 | Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi! |
| |
| 7 | Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo! |
| |
| 8 | Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali! |
| |
| 9 | Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini? |
| |
| 10 | Na yakakusanywa yaliomo vifuani? |
| |
| 11 | Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote! |
| |