95 - AT-TIN |
| |
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
| |
| |
| 1 | Naapa kwa tini na zaituni! |
| |
| 2 | Na kwa Mlima wa Sinai! |
| |
| 3 | Na kwa mji huu wenye amani! |
| |
| 4 | Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa. |
| |
| 5 | Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini! |
| |
| 6 | Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha. |
| |
| 7 | Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo? |
| |
| 8 | Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote? |
| |