70 - AL - MAA'RIJ |
| |
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
| |
| |
| 1 | Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea, |
| |
| 2 | Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia - |
| |
| 3 | Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja. |
| |
| 4 | Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu! |
| |
| 5 | Basi subiri kwa subira njema. |
| |
| 6 | Hakika wao wanaiona iko mbali, |
| |
| 7 | Na Sisi tunaiona iko karibu. |
| |
| 8 | Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa. |
| |
| 9 | Na milima itakuwa kama sufi. |
| |
| 10 | Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake. |
| |
| 11 | Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe, |
| |
| 12 | Na mkewe, na nduguye, |
| |
| 13 | Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu, |
| |
| 14 | Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye. |
| |
| 15 | La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa, |
| |
| 16 | Unao babua ngozi ya kichwa! |
| |
| 17 | Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka. |
| |
| 18 | Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi. |
| |
| 19 | Hakika mtu ameumbwa na papara. |
| |
| 20 | Inapo mgusa shari hupapatika. |
| |
| 21 | Na inapo mgusa kheri huizuilia. |
| |
| 22 | Isipo kuwa wanao sali, |
| |
| 23 | Ambao wanadumisha Sala zao, |
| |
| 24 | Na ambao katika mali yao iko haki maalumu |
| |
| 25 | Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba; |
| |
| 26 | Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo, |
| |
| 27 | Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi. |
| |
| 28 | Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo. |
| |
| 29 | Na ambao wanahifadhi tupu zao. |
| |
| 30 | Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi - |
| |
| 31 | Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka. |
| |
| 32 | Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao, |
| |
| 33 | Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao, |
| |
| 34 | Na ambao wanazihifadhi Sala zao. |
| |
| 35 | Hao ndio watakao hishimiwa Peponi. |
| |
| 36 | Wana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho tu? |
| |
| 37 | Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto! |
| |
| 38 | Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema? |
| |
| 39 | La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua. |
| |
| 40 | Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza |
| |
| 41 | Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi. |
| |
| 42 | Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa, |
| |
| 43 | Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo, |
| |
| 44 | Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyo kuwa wakiahidiwa. |
| |