1 - AL-FAATIH'A |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
2 | Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote; |
|
3 | Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu; |
|
4 | Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo. |
|
5 | Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada. |
|
6 | Tuongoe njia iliyo nyooka, |
|
7 | Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea. |
|