89 - AL - FAJR |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Naapa kwa alfajiri, |
|
2 | Na kwa masiku kumi, |
|
3 | Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja, |
|
4 | Na kwa usiku unapo pita, |
|
5 | Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili? |
|
6 | Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di? |
|
7 | Wa Iram, wenye majumba marefu? |
|
8 | Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi? |
|
9 | Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni? |
|
10 | Na Firauni mwenye vigingi? |
|
11 | Ambao walifanya jeuri katika nchi? |
|
12 | Wakakithirisha humo ufisadi? |
|
13 | Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu. |
|
14 | Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia. |
|
15 | Ama mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu! |
|
16 | Na ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge! |
|
17 | Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima, |
|
18 | Wala hamhimizani kulisha masikini; |
|
19 | Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa, |
|
20 | Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi. |
|
21 | Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande, |
|
22 | Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu, |
|
23 | Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini? |
|
24 | Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu! |
|
25 | Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake. |
|
26 | Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake. |
|
27 | Ewe nafsi iliyo tua! |
|
28 | Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha. |
|
29 | Basi ingia miongoni mwa waja wangu, |
|
30 | Na ingia katika Pepo yangu. |
|