26 - ASH-SHUA'RAA |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | T'aa Siin Miim. (T'.S.M.) |
|
2 | Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha. |
|
3 | Huenda labda ukajikera nafsi yako kwa kuwa hawawi Waumini. |
|
4 | Tunge penda tungeli wateremshia kutoka mbinguni Ishara zikanyenyekea shingo zao. |
|
5 | Wala hauwafikii ukumbusho mpya kutoka kwa Arrahman ila wao hujitenga nao. |
|
6 | Kwa yakini wamekanusha; kwa hivyo zitakuja wafikia khabari za yale waliyo kuwa wakiyafanyia mzaha. |
|
7 | Je! Hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri? |
|
8 | Hakika katika haya zipo Ishara. Lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini. |
|
9 | Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. |
|
10 | Na Mola wako Mlezi, alipo mwita Musa, akamwambia: Fika kwa watu madhaalimu, |
|
11 | Watu wa Firauni. Hawaogopi? |
|
12 | Akasema: Hakika mimi nachelea wasinikanushe. |
|
13 | Na kifua changu kina dhiki, na ulimi wangu haukunjuki vyema. Basi mtumie ujumbe Harun. |
|
14 | Na wao wana kisasi juu yangu, kwa hivyo naogopa wasije kuniuwa. |
|
15 | Akasema: Siyo hivyo kabisa! Nendeni na miujiza yetu. Hakika Sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza. |
|
16 | Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
|
17 | Waachilie Wana wa Israili wende nasi. |
|
18 | (Firauni) akasema: Sisi hatukukulea wewe utotoni, na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi? |
|
19 | Na ukatenda kitendo chako ulicho tenda, nawe ukawa miongoni mwa wasio na shukrani? |
|
20 | (Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipo kuwa miongoni mwa wale walio potea. |
|
21 | Basi nikakukimbieni nilipo kuogopeni, tena Mola wangu Mlezi akanitunukia hukumu, na akanijaalia niwe miongoni mwa Mitume. |
|
22 | Na hiyo ndiyo neema ya kunisumbulia, na wewe umewatia utumwani Wana wa Israili? |
|
23 | Firauni akasema: Na nani huyo Mola Mlezi wa walimwengu wote? |
|
24 | Akasema: Ndiye Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi ni wenye yakini. |
|
25 | (Firauni) akawaambia walio mzunguka: Hamsikilizi? |
|
26 | (Musa) akasema: Ndiye Mola wenu Mlezi, na Mola Mlezi wa baba zenu wa kwanza. |
|
27 | (Firauni) akasema: Hakika huyu Mtume wenu aliye tumwa kwenu ni mwendawazimu. |
|
28 | (Musa) akasema: Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki na Magharibi na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi mnatia akilini. |
|
29 | (Firauni) akasema: Ukimfuata mungu mwengine asiye kuwa mimi, basi bila ya shaka nitakufunga gerezani. |
|
30 | Akasema: Je! Ijapo kuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi? |
|
31 | Akasema: Kilete basi, kama wewe ni katika wasemao kweli. |
|
32 | Basi akaitupa fimbo yake, mara ikawa nyoka wa kuonekana dhaahiri. |
|
33 | Na akautoa mkono wake, na mara ukawa mweupe kwa watazamao. |
|
34 | (Firauni) akawaambia waheshimiwa walio mzunguka: Hakika huyu ni mchawi mtaalamu. |
|
35 | Anataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wake. Basi mna shauri gani? |
|
36 | Wakasema: Mpe muda yeye na nduguye na uwatume mijini wapigao mbiu ya mgambo. |
|
37 | Wakuletee kila mchawi bingwa mtaalamu. |
|
38 | Basi wakakusanywa wachawi wakati na siku maalumu. |
|
39 | Na watu wakaambiwa: Je! Mtakusanyika? |
|
40 | Huenda tutawafuata wachawi wakiwa wao ndio watakao shinda. |
|
41 | Basi walipo kuja wachawi wakamwambia Firauni: Je! Tutapata ujira tukiwa sisi ndio tulio shinda? |
|
42 | Naam! Na hakika mtakuwa katika watu wa mbele. |
|
43 | Musa akwaambia: Tupeni mnavyo taka kutupa. |
|
44 | Basi wakatupa kamba zao na fimbo zao, na wakasema: Kwa nguvu za Firauni hakika sisi hapana shaka ni wenye kushinda. |
|
45 | Musa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizua. |
|
46 | Hapo wachawi walipinduka wakasujudu. |
|
47 | Wakasema: Tunamuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
|
48 | Mola Mlezi wa Musa na Harun. |
|
49 | (Firauni) akasema: Je! Mmemuamini kabla sijakuruhusuni? Bila ya shaka yeye basi ndiye mkubwa wenu aliye kufunzeni uchawi. Basi mtakuja jua! Nitakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakubandikeni misalabani nyote. |
|
50 | Wakasema: Haidhuru, kwani sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. |
|
51 | Hakika sisi tunatumai Mola wetu Mlezi atatusamehe makosa yetu, kwa kuwa ndio wa kwanza wa kuamini. |
|
52 | Na tulimuamrisha Musa kwa wahyi: Nenda na waja wangu wakati wa usiku. Kwa hakika mtafuatwa. |
|
53 | Basi Firauni akawatuma mijini wapiga mbiu za mgambo. |
|
54 | (Wakieneza): Hakika hawa ni kikundi kidogo. |
|
55 | Nao wanatuudhi. |
|
56 | Na sisi ni wengi, wenye kuchukua hadhari. |
|
57 | Basi tukawatoa katika mabustani na chemchem, |
|
58 | Na makhazina, na vyeo vya hishima, |
|
59 | Kadhaalika; na tukawarithisha hayo Wana wa Israili. |
|
60 | Basi wakawafuata lilipo chomoza jua. |
|
61 | Na yalipo onana majeshi mawili haya, watuwa Musa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumepatikana! |
|
62 | (Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa! |
|
63 | Tulimletea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa. |
|
64 | Na tukawajongeza hapo wale wengine. |
|
65 | Tukawaokoa Musa na walio kuwa pamoja naye wote. |
|
66 | Kisha tukawazamisha hao wengine. |
|
67 | Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara; lakini wengi wao si katika wenye kuamini. |
|
68 | Na kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. |
|
69 | Na wasomee khabari za Ibrahim. |
|
70 | Alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Mnaabudu nini? |
|
71 | Wakasema: Tunaabudu masanamu, daima tunayanyenyekea. |
|
72 | Akasema: Je! Yanakusikieni mnapo yaita? |
|
73 | Au yanakufaeni, au yanakudhuruni? |
|
74 | Wakasema: Bali tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo hivyo. |
|
75 | Je! Mmewaona hawa mnao waabudu- |
|
76 | Nyinyi na baba zenu wa zamani? |
|
77 | Kwani hakika hao ni adui zangu, isipo kuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
|
78 | Ambaye ndiye aliye niumba, na Yeye ndiye ananiongoa, |
|
79 | Na ambaye ndiye ananilisha na kuninywesha. |
|
80 | Na ninapo ugua ni Yeye ndiye anaye niponesha. |
|
81 | Na ambaye atanifisha, na kisha atanihuisha. |
|
82 | Na ambaye ndiye ninaye mtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya Malipo. |
|
83 | 83, Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema. |
|
84 | Na unijaalie nitajwe kwa wema na watu watakao kuja baadaye. |
|
85 | Na unijaalie katika warithi wa Bustani za neema. |
|
86 | Na umsamehe baba yangu, kwani hakika alikuwa miongoni mwa wapotovu. |
|
87 | Wala usinihizi Siku watapo fufuliwa. |
|
88 | Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana. |
|
89 | Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi. |
|
90 | Na Pepo itasogezwa kwa wachamngu. |
|
91 | Na Jahannamu itadhihirishwa kwa wapotovu. |
|
92 | Na wataambiwa: Wako wapi mlio kuwa mkiwaabudu |
|
93 | Badala ya Mwenyezi Mungu? Je! Wanakusaidieni, au wanajisaidia wenyewe? |
|
94 | Basi watavurumizwa humo wao na hao wakosefu, |
|
95 | Na majeshi ya Ibilisi yote. |
|
96 | Watasema, na hali ya kuwa wanazozana humo: |
|
97 | Wallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio dhaahiri, |
|
98 | Tulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
|
99 | Na hawakutupoteza ila wale wakosefu. |
|
100 | Basi hatuna waombezi. |
|
101 | Wala rafiki wa dhati. |
|
102 | Laiti tungeli pata kurejea tena tungeli kuwa katika Waumini. |
|
103 | Hakika katika haya ipo Ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini. |
|
104 | Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. |
|
105 | Kaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume. |
|
106 | Alipo waambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamchimngu? |
|
107 | Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. |
|
108 | Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. |
|
109 | Na sikutakini juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
|
110 | Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. |
|
111 | Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanao kufuata ni watu wa chini? |
|
112 | Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya? |
|
113 | Hisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua! |
|
114 | Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini. |
|
115 | Mimi si cho chote ila ni Mwonyaji wa dhaahiri shaahiri. |
|
116 | Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe. |
|
117 | Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha. |
|
118 | Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini. |
|
119 | Kwa hivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika marikebu iliyo sheheni. |
|
120 | Kisha tukawazamisha baadaye walio bakia. |
|
121 | Hakika katika haya ipo Ishara, lakini si wengi wao walio kuwa Waumini. |
|
122 | Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. |
|
123 | Kina A'd waliwakanusha Mitume. |
|
124 | Alipo waambia ndugu yao, Hud: Je! Hamchimngu? |
|
125 | Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. |
|
126 | Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. |
|
127 | Wala sikutakeni juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
|
128 | Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi? |
|
129 | Na mnajenga majengo ya fakhari kama kwamba mtaishi milele! |
|
130 | Na mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari. |
|
131 | Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini. |
|
132 | Na mcheni aliye kupeni haya mnayo yajua. |
|
133 | Amekupeni wanyama wa kufuga na wana. |
|
134 | Na mabustani na chemchem. |
|
135 | Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa. |
|
136 | Wakasema: Ni mamoja kwetu, ukitupa mawaidha au hukuwa miongoni mwa watoao mawaidha. |
|
137 | Haya si chochote ila ni mtindo wa watu wa tokea zamani. |
|
138 | Wala sisi hatutaadhibiwa. |
|
139 | Wakamkanusha; nasi tukawaangamiza. Hakika bila ya shaka katika haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. |
|
140 | Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. |
|
141 | Kina Thamud waliwakanusha Mitume. |
|
142 | Alipo waambia ndugu yao Saleh: Je! Hamumchimngu? |
|
143 | Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. |
|
144 | Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini. |
|
145 | Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
|
146 | Je! Mtaachwa salama usalimina katika haya yaliyopo hapa? |
|
147 | Katika mabustani, na chemchem? |
|
148 | Na konde na mitende yenye makole yaliyo wiva. |
|
149 | Na mnachonga milimani majumba kwa ustadi. |
|
150 | Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. |
|
151 | 151, Wala msit'ii amri za walio pindukia mipaka, |
|
152 | Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi. |
|
153 | Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa walio rogwa. |
|
154 | Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi lete Ishara ukiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli. |
|
155 | Akasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa, na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalumu. |
|
156 | Wala msimguse kwa uwovu, isije ikakushikeni adhabu ya Siku Kubwa. |
|
157 | Lakini wakamuuwa, na wakawa wenye kujuta. |
|
158 | Basi ikawapata adhabu. Hakika katika hayo ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. |
|
159 | Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. |
|
160 | Watu wa Lut'i waliwakanusha Mitume. |
|
161 | Alipo waambia ndugu yao, Lut'i: Je! Hamumchimngu? |
|
162 | Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu kwenu. |
|
163 | Basi mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi. |
|
164 | Wala mimi sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
|
165 | Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume? |
|
166 | Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka! |
|
167 | Wakasema: Ewe Lut'i! Usipo acha, hapana shaka utakuwa miongoni mwa wanao tolewa mji! |
|
168 | Akasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukia hichi kitendo chenu. |
|
169 | Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo. |
|
170 | Basi tukamwokoa yeye na ahali zake wote, |
|
171 | Isipo kuwa kikongwe katika walio kaa nyuma. |
|
172 | Kisha tukawaangamiza wale wengine. |
|
173 | Na tukawanyeshea mvua, basi ni ovu mno mvua ya waliyo onywa. |
|
174 | Hakika katika hayo ipo Ishara. Na hawakuwa wengi wao wenye kuamini. |
|
175 | Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. |
|
176 | Watu wa Machakani waliwakanusha Mitume. |
|
177 | Shuaibu alipo waambia: Je! Hamfanyi mkamchamngu? |
|
178 | Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. |
|
179 | Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. |
|
180 | Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
|
181 | Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja. |
|
182 | Na pimeni kwa haki iliyo nyooka; |
|
183 | Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi. |
|
184 | Na mcheni aliye kuumbeni nyinyi na vizazi vilivyo tangulia. |
|
185 | Wakasema: Hakika wewe ni katika walio rogwa. |
|
186 | Na wewe si chochote ila ni mtu tu kama sisi, na kwa yakini tunakuona wewe ni katika waongo. |
|
187 | Hebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli. |
|
188 | Akasema: Mola wangu Mlezi anajua zaidi mnayo yatenda. |
|
189 | Basi walimkanusha, na ikawashika adhabu ya siku ya kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa. |
|
190 | Hakika katika hayo ipo Ishara, lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. |
|
191 | Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. |
|
192 | Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
|
193 | Ameuteremsha Roho muaminifu, |
|
194 | Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji, |
|
195 | Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi. |
|
196 | Na hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya kale. |
|
197 | Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili? |
|
198 | Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu, |
|
199 | Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini. |
|
200 | Namna hivi tunaingiza katika nyoyo za wakosefu. |
|
201 | Hawataiamini mpaka waione adhabu chungu. |
|
202 | Basi itawafikia kwa ghafla, na hali hawana khabari. |
|
203 | Na watasema: Je, tutapewa muhula? |
|
204 | Basi, je, wanaihimiza adhabu yetu? |
|
205 | Waonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka, |
|
206 | Kisha yakawafikia waliyo kuwa wakiahidiwa, |
|
207 | Yatawafaa nini yale waliyo stareheshewa? |
|
208 | Wala hatukuangamiza mji wo wote ila ulikuwa na waonyaji - |
|
209 | Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu. |
|
210 | Wala Mashet'ani hawakuteremka nayo, |
|
211 | Wala haitakiwi kwao, na wala hawawezi. |
|
212 | Hakika hao wametengwa na kusikia. |
|
213 | Basi usimwombe mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ukawa miongoni mwa watakao adhibiwa. |
|
214 | Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe. |
|
215 | Na watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwa Waumini. |
|
216 | Na ikiwa watakuasi basi sema: Mimi najitenga mbali na hayo mnayo yatenda. |
|
217 | Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. |
|
218 | Ambaye anakuona unapo simama, |
|
219 | Na mageuko yako kati ya wanao sujudu. |
|
220 | Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua. |
|
221 | Je! Nikwambieni nani wanawashukia Mashet'ani? |
|
222 | Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi. |
|
223 | Wanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi wao ni waongo. |
|
224 | Na watungaji mashairi ni wapotofu ndio wanawafuata. |
|
225 | Je! Huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde? |
|
226 | Na kwamba wao husema wasiyo yatenda? |
|
227 | Isipo kuwa wale walio amini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea wanapo dhulumiwa. Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka. |
|