90 - AL - BALAD |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Naapa kwa Mji huu! |
|
2 | Nawe unaukaa Mji huu. |
|
3 | Na naapa kwa mzazi na alicho kizaa. |
|
4 | Hakika tumemuumba mtu katika taabu. |
|
5 | Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza? |
|
6 | Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali. |
|
7 | Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona? |
|
8 | Kwani hatukumpa macho mawili? |
|
9 | Na ulimi, na midomo miwili? |
|
10 | Na tukambainishia zote njia mbili? |
|
11 | Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. |
|
12 | Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani? |
|
13 | Kumkomboa mtumwa; |
|
14 | Au kumlisha siku ya njaa |
|
15 | Yatima aliye jamaa, |
|
16 | Au masikini aliye vumbini. |
|
17 | Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana. |
|
18 | Hao ndio watu wa kheri wa kuliani. |
|
19 | Lakini walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. |
|
20 | Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande. |
|