69 - AL - H'AAQQAH |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Tukio la haki. |
|
2 | Nini hilo Tukio la haki? |
|
3 | Na nini kitakujuulisha nini hilo Tukio la haki? |
|
4 | Thamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unao situsha. |
|
5 | Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno. |
|
6 | Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usio zuilika. |
|
7 | Alio wapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani. |
|
8 | Basi je! Unamwona mmoja wao aliye baki? |
|
9 | Na Firauni na walio mtangulia, na miji iliyo pinduliwa chini juu, walileta khatia. |
|
10 | Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu. |
|
11 | Maji yalipo furika Sisi tulikupandisheni katika safina, |
|
12 | Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalo sikia liyahifadhi. |
|
13 | Na litapo pulizwa barugumu mpulizo mmoja tu, |
|
14 | Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja, |
|
15 | Siku hiyo ndio Tukio litatukia. |
|
16 | Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa. |
|
17 | Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi. |
|
18 | Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu. |
|
19 | Basi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu! |
|
20 | Hakika nalijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu. |
|
21 | Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza, |
|
22 | Katika Bustani ya juu, |
|
23 | Matunda yake yakaribu. |
|
24 | Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita. |
|
25 | Na ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu! |
|
26 | Wala nisingeli jua nini hisabu yangu. |
|
27 | Laiti mauti ndiyo yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa. |
|
28 | Mali yangu hayakunifaa kitu. |
|
29 | Madaraka yangu yamenipotea. |
|
30 | (Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu! |
|
31 | Kisha mtupeni Motoni! |
|
32 | Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini! |
|
33 | Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, |
|
34 | Wala hahimizi kulisha masikini. |
|
35 | Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu, |
|
36 | Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni. |
|
37 | Chakula hicho hawakili ila wakosefu. |
|
38 | Basi naapa kwa mnavyo viona, |
|
39 | Na msivyo viona, |
|
40 | Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima. |
|
41 | Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini. |
|
42 | Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka. |
|
43 | Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
|
44 | Na lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu, |
|
45 | Bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia, |
|
46 | Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo! |
|
47 | Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeli weza kutuzuia. |
|
48 | Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wachamngu. |
|
49 | Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha. |
|
50 | Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanao kataa. |
|
51 | Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini. |
|
52 | Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu. |
|