93 - WADH-DHUH'AA |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Naapa kwa mchana! |
|
2 | Na kwa usiku unapo tanda! |
|
3 | Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe. |
|
4 | Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia. |
|
5 | Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike. |
|
6 | Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi? |
|
7 | Na akakukuta umepotea akakuongoa? |
|
8 | Akakukuta mhitaji akakutosheleza? |
|
9 | Basi yatima usimwonee! |
|
10 | Na anaye omba au kuuliza usimkaripie! |
|
11 | Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie. |
|