91 - ASH-SHAMS |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Naapa kwa jua na mwangaza wake! |
|
2 | Na kwa mwezi unapo lifuatia! |
|
3 | Na kwa mchana unapo lidhihirisha! |
|
4 | Na kwa usiku unapo lifunika! |
|
5 | Na kwa mbingu na kwa aliye ijenga! |
|
6 | Na kwa ardhi na kwa aliye itandaza! |
|
7 | Na kwa nafsi na kwa aliye itengeneza! |
|
8 | Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake, |
|
9 | Hakika amefanikiwa aliye itakasa, |
|
10 | Na hakika amekhasiri aliye iviza. |
|
11 | Kina Thamudi walikadhibisha kwa sababu ya upotofu wao, |
|
12 | Alipo simama mwovu wao mkubwa, |
|
13 | Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipo waambia: Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu, mwacheni anywe maji fungu lake. |
|
14 | Lakini walimkadhibisha na wakamchinja ngamia, kwa hivyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao na akawafuta kabisa. |
|
15 | Wala Yeye haogopi matokeo yake. |
|