___Translations___

_Quran?_

_Gadgets_

_Search_

_Links_

_Contribute_

_Note_

1 - AL-FAATIH'A
2 - AL - BAQARA
3 - AL I'MRAN
4 - AN-NISAAI
5 - AL - MAIDA
6 - AL - AN-A'AM
7 - AL - A'RAAF
8 - AL - ANFAAL
9 - AT-TAWBA
10 - YUNUS
11 - HUD
12 - YUSUF
13 - AR-RAA'D
14 - IBRAHIM
15 - AL - HIJR
16 - AN NAH'L
17 - AL ISRAAI (BANI ISRAIL)
18 - AL - KAHF
19 - MARYAM
20 - T'AHA
21 - AL - ANBIYAA
22 - AL -HAJJ
23 - AL - MUUMINUN
24 - AN - NUR
25 - AL - FURQAN
26 - ASH-SHUA'RAA
27 - AN-NAML
28 - AL-QAS'AS'
29 - AL - A'NKABUT
30 - AR-RUM
31 - LUQMAN
32 - ASSAJDAH
33 - AL-AH'ZAB
34 - SABAA
35 - FAAT'IR
36 - YA-SIN
37 - ASS'AFFAT
38 - S'AAD
39 - AZZUMAR
40 - GHAAFIR (AU AL MUUMIN)
41 - FUSS'ILAT (AU H'A MIM SAJDAH)
42 - ASH-SHUURA
43 - AZZUKHRUF
44 - ADDUKHAN
45 - AL - JAATHIYA
46 - AL - AH'QAAF
47 - MUH'AMMAD
48 - AL FAT-H'I
49 - AL H'UJURAAT
50 - QAAF
51 - ADH-DHAARIYAAT
52 - ATT'UR
53 - ANNAJM
54 - AL-QAMAR
55 - ARRAH'MAN
56 - AL -WAAQIA'H
57 - AL -H'ADIID
58 - AL - MUJAADALAH
59 - AL - H'ASHRI
60 - AL - MUMTAH'INAH
61 - ASS'AF
62 - AL - JUMUA'
63 - AL - MUNAAFIQUN
64 - ATTAGHAABUN
65 - ATT'ALAAQ
66 - ATTAH'RIIM
67 - AL - MULK
68 - AL - QALAM
69 - AL - H'AAQQAH
70 - AL - MAA'RIJ
71 - NUH'
72 - AL - JINN
73 - AL - MUZZAMMIL
74 - AL - MUDDATHTHIR
75 - AL - QIYAMAH
76 - AL - INSAN
77 - AL - MURSALAAT
78 - ANNABAA
79 - ANNAZIA'AT
80 - A'BASA
81 - ATTAKWIR
82 - AL - INFIT'AAR
83 - AL - MUT'AFFIFIIN
84 - AL - INSHIQAAQ
85 - AL - BURUUJ
86 - ATT'AARIQ
87 - AL - AA'LAA
88 - AL - GHAASHIYAH
89 - AL - FAJR
90 - AL - BALAD
91 - ASH-SHAMS
92 - AL - LAYL
93 - WADH-DHUH'AA
94 - ASH-SHARH'
95 - AT-TIN
96 - AL - A'LAQ
97 - AL - QADR
98 - AL - BAYYINAH
99 - AZ-ZILZALAH
100 - AL - A'ADIYAAT
101 - AL - QAARIA'H
102 - AT-TAKAATHUR
103 - AL - A'S'R
104 - AL - HUMAZAH
105 - AL - FIIL
106 - QURAISH
107 - AL - MAAU'N
108 - AL - KAWTHAR
109 - AL - KAFIRUN
110 - ANNAS'R
111 - AL - MASAD
112 - AL - IKHLAS'
113 - AL - FALAQ
114 - ANNAS
KISWAHILI

44 - ADDUKHAN

 

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 
1H'a Mim
 
2Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha,
 
3Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji.
 
4Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima,
 
5Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma.
 
6Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.
 
7Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini.
 
8Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo.
 
9Lakini wao wanacheza katika shaka.
 
10Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapo leta moshi ulio dhaahiri,
 
11Utakao wafunika watu: Hii ni adhabu chungu!
 
12Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini.
 
13Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha.
 
14Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu.
 
15Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile!
 
16Siku tutayo yashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa.
 
17Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu.
 
18Akasema: Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu.
 
19Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi.
 
20Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe.
 
21Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami.
 
22Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: Hakika watu hawa ni wakosefu.
 
23Mwenyezi Mungu akasema: Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa.
 
24Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao hao ni jeshi litakalo zamishwa.
 
25Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha!
 
26Na mimea na vyeo vitukufu!
 
27Na neema walizo kuwa wakijistareheshea!
 
28Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe.
 
29La mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula.
 
30Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha,
 
31Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka.
 
32Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe.
 
33Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi.
 
34Hakika hawa wanasema:
 
35Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi.
 
36Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.
 
37Je! Ni wao bora au watu wa Tubbaa' na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu.
 
38Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo.
 
39Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui.
 
40Hakika siku ya Uamuzi ni wakati ulio wekwa kwa wao wote.
 
41Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa.
 
42Isipo kuwa atakaye mrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.
 
43Hakika Mti wa Zaqqum,
 
44Ni chakula cha mwenye dhambi.
 
45Kama shaba iliyo yayushwa, hutokota matumboni
 
46Kama kutokota kwa maji ya moto.
 
47(Itasemwa:) Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu!
 
48Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayo chemka.
 
49Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu!
 
50Hakika haya ndiyo mliyo kuwa mkiyatilia shaka.
 
51Hakika wachamngu watakuwa katika mahali pa amani,
 
52Katika mabustani na chemchem,
 
53Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana,
 
54Hivi ndivyo itakavyo kuwa, na tutawaoza mahurilaini.
 
55Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani.
 
56Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu,
 
57Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
 
58Basi tumeifanya nyepesi hii Qur'ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka.
 
59Ngoja tu, na wao wangoje pia.