111 - AL - MASAD |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia. |
|
2 | Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma. |
|
3 | Atauingia Moto wenye mwako. |
|
4 | Na mkewe, mchukuzi wa kuni, |
|
5 | Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa. |
|