87 - AL - AA'LAA |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa, |
|
2 | Aliye umba, na akaweka sawa, |
|
3 | Na ambaye amekadiria na akaongoa, |
|
4 | Na aliye otesha malisho, |
|
5 | Kisha akayafanya makavu, meusi. |
|
6 | Tutakusomesha wala hutasahau, |
|
7 | Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana. |
|
8 | Na tutakusahilishia yawe mepesi. |
|
9 | Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa. |
|
10 | Atakumbuka mwenye kuogopa. |
|
11 | Na atajitenga mbali nayo mpotovu, |
|
12 | Ambaye atauingia Moto mkubwa. |
|
13 | Tena humo hatakufa wala hawi hai. |
|
14 | Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa. |
|
15 | Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali. |
|
16 | Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia! |
|
17 | Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi. |
|
18 | Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo, |
|
19 | Vitabu vya Ibrahimu na Musa. |
|