75 - AL - QIYAMAH |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Ninaapa kwa Siku ya Kiyama! |
|
2 | Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu! |
|
3 | Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake? |
|
4 | Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake! |
|
5 | Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake. |
|
6 | Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama? |
|
7 | Basi jicho litapo dawaa, |
|
8 | Na mwezi utapo patwa, |
|
9 | Na likakusanywa jua na mwezi, |
|
10 | Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio? |
|
11 | La! Hapana pa kukimbilia! |
|
12 | Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu. |
|
13 | Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha. |
|
14 | Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake. |
|
15 | Na ingawa atatoa chungu ya udhuru. |
|
16 | Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka. |
|
17 | Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha. |
|
18 | Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake. |
|
19 | Kisha ni juu yetu kuubainisha. |
|
20 | Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani, |
|
21 | Na mnaacha maisha ya Akhera. |
|
22 | Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara, |
|
23 | Zinamwangallia Mola wao Mlezi. |
|
24 | Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana. |
|
25 | Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo. |
|
26 | La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo, |
|
27 | Na pakasemwa: Nani wa kumganga? |
|
28 | Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki; |
|
29 | Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi, |
|
30 | Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi! |
|
31 | Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali. |
|
32 | Bali alikanusha, na akageuka. |
|
33 | Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao. |
|
34 | Ole wako, ole wako! |
|
35 | Kisha Ole wako, ole wako! |
|
36 | Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure? |
|
37 | Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa? |
|
38 | Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo. |
|
39 | Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke. |
|
40 | Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu? |
|