88 - AL - GHAASHIYAH |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza? |
|
2 | Siku hiyo nyuso zitainama, |
|
3 | Zikifanya kazi, nazo taabani. |
|
4 | Ziingie katika Moto unao waka - |
|
5 | Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka. |
|
6 | Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba. |
|
7 | Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa. |
|
8 | Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu. |
|
9 | Zitakuwa radhi kwa juhudi yao, |
|
10 | Katika Bustani ya juu. |
|
11 | Hawatasikia humo upuuzi. |
|
12 | Humo imo chemchem inayo miminika. |
|
13 | Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa, |
|
14 | Na bilauri zilizo pangwa, |
|
15 | Na matakia safu safu, |
|
16 | Na mazulia yaliyo tandikwa. |
|
17 | Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa? |
|
18 | Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa? |
|
19 | Na milima jinsi ilivyo thibitishwa? |
|
20 | Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa? |
|
21 | Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji. |
|
22 | Wewe si mwenye kuwatawalia. |
|
23 | Lakini anaye rudi nyuma na kukataa, |
|
24 | Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa! |
|
25 | Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao. |
|
26 | Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao! |
|