77 - AL - MURSALAAT |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole! |
|
2 | Na zinazo vuma kwa kasi! |
|
3 | Na zikaeneza maeneo yote! |
|
4 | Na zinazo farikisha zikatawanya! |
|
5 | Na zinazo peleka mawaidha! |
|
6 | Kwa kuudhuru au kuonya, |
|
7 | Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa! |
|
8 | Wakati nyota zitakapo futwa, |
|
9 | Na mbingu zitakapo pasuliwa, |
|
10 | Na milima itakapo peperushwa, |
|
11 | Na Mitume watakapo wekewa wakati wao, |
|
12 | Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo? |
|
13 | Kwa siku ya kupambanua! |
|
14 | Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini? |
|
15 | Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha! |
|
16 | Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia? |
|
17 | Kisha tukawafuatilizia walio fuatia? |
|
18 | Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu! |
|
19 | Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
|
20 | Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa? |
|
21 | Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti? |
|
22 | Mpaka muda maalumu? |
|
23 | Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria. |
|
24 | Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
|
25 | Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya |
|
26 | Walio hai na maiti? |
|
27 | Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu? |
|
28 | Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
|
29 | Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha! |
|
30 | Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu! |
|
31 | Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako. |
|
32 | Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba! |
|
33 | Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano! |
|
34 | Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
|
35 | Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu, |
|
36 | Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru. |
|
37 | Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! |
|
38 | Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia. |
|
39 | Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi! |
|
40 | Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! |
|
41 | Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem, |
|
42 | Na matunda wanayo yapenda, |
|
43 | Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda. |
|
44 | Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema. |
|
45 | Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
|
46 | Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu! |
|
47 | Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
|
48 | Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami. |
|
49 | Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! |
|
50 | Basi maneno gani baada ya haya watayaamini? |
|