84 - AL - INSHIQAAQ |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Itapo chanika mbingu, |
|
2 | Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza, |
|
3 | Na ardhi itakapo tanuliwa, |
|
4 | Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu, |
|
5 | Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza, |
|
6 | Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta. |
|
7 | Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia, |
|
8 | Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi, |
|
9 | Na arudi kwa ahali zake na furaha. |
|
10 | Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake, |
|
11 | Basi huyo ataomba kuteketea. |
|
12 | Na ataingia Motoni. |
|
13 | Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake. |
|
14 | Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena. |
|
15 | Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona! |
|
16 | Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa, |
|
17 | Na kwa usiku na unavyo vikusanya, |
|
18 | Na kwa mwezi unapo pevuka, |
|
19 | Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka! |
|
20 | Basi wana nini hawaamini? |
|
21 | Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu? |
|
22 | Bali walio kufuru wanakanusha tu. |
|
23 | Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria. |
|
24 | Basi wabashirie adhabu chungu! |
|
25 | Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika. |
|