102 - AT-TAKAATHUR |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Kumekushughulisheni kutafuta wingi, |
|
2 | Mpaka mje makaburini! |
|
3 | Sivyo hivyo! Mtakuja jua! |
|
4 | 4, Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua! |
|
5 | Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini, |
|
6 | Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu! |
|
7 | Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini. |
|
8 | Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema. |
|