96 - AL - A'LAQ |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, |
|
2 | Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, |
|
3 | Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! |
|
4 | Ambaye amefundisha kwa kalamu. |
|
5 | Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui. |
|
6 | Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri |
|
7 | Akijiona katajirika. |
|
8 | Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo. |
|
9 | Umemwona yule anaye mkataza |
|
10 | Mja anapo sali? |
|
11 | Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu? |
|
12 | Au anaamrisha uchamngu? |
|
13 | Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma? |
|
14 | Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona? |
|
15 | Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele! |
|
16 | Shungi la uwongo, lenye makosa! |
|
17 | Basi na awaite wenzake! |
|
18 | Nasi tutawaita Mazabania! |
|
19 | Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee! |
|