79 - ANNAZIA'AT |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Naapa kwa wanao komoa kwa nguvu, |
|
2 | Na kwa wanao toa kwa upole, |
|
3 | Na wanao ogelea, |
|
4 | Wakishindana mbio, |
|
5 | Wakidabiri mambo. |
|
6 | Siku kitapo tetemeka cha kutetemeka, |
|
7 | Kifuate cha kufuatia. |
|
8 | Siku hiyo nyoyo zitapiga piga, |
|
9 | Macho yatainama chini. |
|
10 | Sasa wanasema: Ati kweli tutarudishwa kwenye hali ya kwanza? |
|
11 | Hata tukiwa mifupa iliyo bunguliwa? |
|
12 | Wanasema: Basi marejeo hayo ni yenye khasara! |
|
13 | Kwa hakika hayo ni ukelele mmoja tu, |
|
14 | Mara watakuwa kwenye uwanda wa mkutano! |
|
15 | Je! Imekufikia hadithi ya Musa? |
|
16 | Mola wake Mlezi alipo mwita katika bonde takatifu la T'uwaa, akamwambia: |
|
17 | Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amezidi jeuri. |
|
18 | Umwambie: Je! Unapenda kujitakasa? |
|
19 | Nami nitakuongoa ufike kwa Mola wako Mlezi, upate kumcha. |
|
20 | Basi alimwonyesha Ishara kubwa. |
|
21 | Lakini aliikadhibisha na akaasi. |
|
22 | Kisha alirudi nyuma, akaingia kufanya juhudi. |
|
23 | Akakusanya watu akanadi. |
|
24 | Akasema: Mimi ndiye Mola wenu Mlezi mkuu kabisa. |
|
25 | Basi hapo Mwenyezi Mungu akamshika kumuadhibu kwa la mwisho na la mwanzo. |
|
26 | Kwa hakika katika haya yapo mazingatio kwa wanao ogopa. |
|
27 | Je! Ni vigumu zaidi kukuumbeni nyinyi au mbingu? Yeye ndiye aliye ijenga! |
|
28 | Akainua kimo chake, na akaitengeneza vizuri. |
|
29 | Na akautia giza usiku wake, na akautokeza mchana wake. |
|
30 | Na juu ya hivyo ameitandaza ardhi. |
|
31 | Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake, |
|
32 | Na milima akaisimamisha, |
|
33 | Kwa nafuu yenu na mifugo yenu. |
|
34 | Basi itakapo fika hiyo balaa kubwa, |
|
35 | Siku ambayo mtu atakumbuka aliyo yafanya, |
|
36 | Na Jahannamu itadhihirishwa kwa mwenye kuona, |
|
37 | Basi ama yule aliye zidi ujeuri, |
|
38 | Na akakhiari maisha ya dunia, |
|
39 | Kwa hakika Jahannamu ndiyo makaazi yake! |
|
40 | Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio, |
|
41 | Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake! |
|
42 | Wanakuuliza Saa (ya Kiyama) itakuwa lini? |
|
43 | Una nini wewe hata uitaje? |
|
44 | Kwa Mola wako Mlezi ndio mwisho wake. |
|
45 | Kwa hakika wewe ni mwonyaji tu kwa mwenye kuikhofu. |
|
46 | Ni kama kwamba wao siku watapo iona (hiyo Saa) hawakukaa ila jioni moja tu, au mchana wake. |
|