82 - AL - INFIT'AAR |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Mbingu itapo chanika, |
|
2 | Na nyota zitapo tawanyika, |
|
3 | Na bahari zitakapo pasuliwa, |
|
4 | Na makaburi yatapo fukuliwa, |
|
5 | Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma. |
|
6 | Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu? |
|
7 | Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha, |
|
8 | Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga. |
|
9 | Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo. |
|
10 | Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu, |
|
11 | Waandishi wenye hishima, |
|
12 | Wanayajua mnayo yatenda. |
|
13 | Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema, |
|
14 | Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni; |
|
15 | Wataingia humo Siku ya Malipo. |
|
16 | Na hawatoacha kuwamo humo. |
|
17 | Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? |
|
18 | Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? |
|
19 | Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu. |
|