104 - AL - HUMAZAH |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Ole wake kila safihi, msengenyaji! |
|
2 | Aliye kusanya mali na kuyahisabu. |
|
3 | Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele! |
|
4 | Hasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama. |
|
5 | Na nani atakujuvya ni nini H'ut'ama? |
|
6 | Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa. |
|
7 | Ambao unapanda nyoyoni. |
|
8 | Hakika huo utafungiwa nao |
|
9 | Kwenye nguzo zilio nyooshwa. |
|