78 - ANNABAA |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | WANAULIZANA nini? |
|
2 | Ile khabari kuu, |
|
3 | Ambayo kwayo wanakhitalifiana. |
|
4 | La! Karibu watakuja jua. |
|
5 | Tena la! Karibu watakuja jua. |
|
6 | Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko? |
|
7 | Na milima kama vigingi? |
|
8 | Na tukakuumbeni kwa jozi? |
|
9 | Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko? |
|
10 | Na tukaufanya usiku ni nguo? |
|
11 | Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha? |
|
12 | Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu? |
|
13 | Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto; |
|
14 | Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni, |
|
15 | Ili tutoe kwayo nafaka na mimea, |
|
16 | Na mabustani yenye miti iliyo kamatana. |
|
17 | Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake, |
|
18 | Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi, |
|
19 | Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango, |
|
20 | Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi. |
|
21 | Hakika Jahannamu inangojea! |
|
22 | Kwa walio asi ndio makaazi yao, |
|
23 | Wakae humo karne baada ya karne, |
|
24 | Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji, |
|
25 | Ila maji yamoto sana na usaha, |
|
26 | Ndio jaza muwafaka. |
|
27 | Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu. |
|
28 | Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu. |
|
29 | Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika. |
|
30 | Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu! |
|
31 | Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu, |
|
32 | Mabustani na mizabibu, |
|
33 | Na wake walio lingana nao, |
|
34 | Na bilauri zilizo jaa, |
|
35 | Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo - |
|
36 | Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha. |
|
37 | Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake! |
|
38 | Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu. |
|
39 | Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi. |
|
40 | Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo! |
|