94 - ASH-SHARH' |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Hatukukunjulia kifua chako? |
|
2 | Na tukakuondolea mzigo wako, |
|
3 | Ulio vunja mgongo wako? |
|
4 | Na tukakunyanyulia utajo wako? |
|
5 | Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi, |
|
6 | Hakika pamoja na uzito upo wepesi. |
|
7 | Na ukipata faragha, fanya juhudi. |
|
8 | Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie. |
|