55 - ARRAH'MAN |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Arrah'man, Mwingi wa Rehema |
|
2 | Amefundisha Qur'ani. |
|
3 | Amemuumba mwanaadamu, |
|
4 | Akamfundisha kubaini. |
|
5 | Jua na mwezi huenda kwa hisabu. |
|
6 | Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea. |
|
7 | Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani, |
|
8 | Ili msidhulumu katika mizani. |
|
9 | Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani. |
|
10 | Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe. |
|
11 | Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba. |
|
12 | Na nafaka zenye makapi, na rehani. |
|
13 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha |
|
14 | Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo.. |
|
15 | Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto. |
|
16 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha |
|
17 | Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili. |
|
18 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
19 | Anaziendesha bahari mbili zikutane; |
|
20 | Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane. |
|
21 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
22 | Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani. |
|
23 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
24 | Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa kama vilima. |
|
25 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
26 | Kila kilioko juu yake kitatoweka. |
|
27 | Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu. |
|
28 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
29 | Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo. |
|
30 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
31 | Tutakuhisabuni enyi makundi mawili. |
|
32 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
33 | Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka. |
|
34 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
35 | Mtapelekewa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda. |
|
36 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
37 | Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta. |
|
38 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
39 | Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini. |
|
40 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
41 | Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu. |
|
42 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
43 | Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha. |
|
44 | Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka. |
|
45 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
46 | Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili. |
|
47 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
48 | Bustani zenye matawi yaliyo tanda. |
|
49 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
50 | Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita. |
|
51 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
52 | Humo katika kila matunda zimo namna mbili. |
|
53 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
54 | Wawe wameegemea matandiko yenye bit'ana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu. |
|
55 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
56 | Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini. |
|
57 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
58 | Kama kwamba wao ni yakuti na marijani. |
|
59 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha. |
|
60 | Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani? |
|
61 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
62 | Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili. |
|
63 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
64 | Za kijani kibivu. |
|
65 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
66 | Na chemchem mbili zinazo furika. |
|
67 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
68 | Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga. |
|
69 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
70 | Humo wamo wanawake wema wazuri. |
|
71 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
72 | Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema. |
|
73 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
74 | Hajawagusa mtu wala jini kabla yao. |
|
75 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
76 | Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri. |
|
77 | Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? |
|
78 | Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu. |
|