85 - AL - BURUUJ |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Naapa kwa mbingu yenye Buruji! |
|
2 | Na kwa siku iliyo ahidiwa! |
|
3 | Na kwa shahidi na kinacho shuhudiwa! |
|
4 | Wameangamizwa watu wa makhandaki |
|
5 | Yenye moto wenye kuni nyingi, |
|
6 | Walipo kuwa wamekaa hapo, |
|
7 | Na wao ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia Waumini. |
|
8 | Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa, |
|
9 | Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shaahidi wa kila kitu. |
|
10 | Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua. |
|
11 | Hakika walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa. |
|
12 | Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali. |
|
13 | Yeye ndiye anaye anzisha na ndiye anaye rejeza tena, |
|
14 | Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi, |
|
15 | Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu, |
|
16 | Atendaye ayatakayo. |
|
17 | Je! Zimekuwasilia khabari za majeshi? |
|
18 | Ya Firauni na Thamudi? |
|
19 | Lakini walio kufuru wamo katika kukadhibisha. |
|
20 | Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka. |
|
21 | Bali hii ni Qur'ani tukufu |
|
22 | Katika Ubao Ulio Hifadhiwa. |
|