101 - AL - QAARIA'H |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Inayo gonga! |
|
2 | Nini Inayo gonga? |
|
3 | Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga? |
|
4 | Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika; |
|
5 | Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa! |
|
6 | Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, |
|
7 | Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza. |
|
8 | Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, |
|
9 | Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya! |
|
10 | Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo? |
|
11 | Ni Moto mkali! |
|