___Translations___

_Quran?_

_Gadgets_

_Search_

_Links_

_Contribute_

_Note_

1 - AL-FAATIH'A
2 - AL - BAQARA
3 - AL I'MRAN
4 - AN-NISAAI
5 - AL - MAIDA
6 - AL - AN-A'AM
7 - AL - A'RAAF
8 - AL - ANFAAL
9 - AT-TAWBA
10 - YUNUS
11 - HUD
12 - YUSUF
13 - AR-RAA'D
14 - IBRAHIM
15 - AL - HIJR
16 - AN NAH'L
17 - AL ISRAAI (BANI ISRAIL)
18 - AL - KAHF
19 - MARYAM
20 - T'AHA
21 - AL - ANBIYAA
22 - AL -HAJJ
23 - AL - MUUMINUN
24 - AN - NUR
25 - AL - FURQAN
26 - ASH-SHUA'RAA
27 - AN-NAML
28 - AL-QAS'AS'
29 - AL - A'NKABUT
30 - AR-RUM
31 - LUQMAN
32 - ASSAJDAH
33 - AL-AH'ZAB
34 - SABAA
35 - FAAT'IR
36 - YA-SIN
37 - ASS'AFFAT
38 - S'AAD
39 - AZZUMAR
40 - GHAAFIR (AU AL MUUMIN)
41 - FUSS'ILAT (AU H'A MIM SAJDAH)
42 - ASH-SHUURA
43 - AZZUKHRUF
44 - ADDUKHAN
45 - AL - JAATHIYA
46 - AL - AH'QAAF
47 - MUH'AMMAD
48 - AL FAT-H'I
49 - AL H'UJURAAT
50 - QAAF
51 - ADH-DHAARIYAAT
52 - ATT'UR
53 - ANNAJM
54 - AL-QAMAR
55 - ARRAH'MAN
56 - AL -WAAQIA'H
57 - AL -H'ADIID
58 - AL - MUJAADALAH
59 - AL - H'ASHRI
60 - AL - MUMTAH'INAH
61 - ASS'AF
62 - AL - JUMUA'
63 - AL - MUNAAFIQUN
64 - ATTAGHAABUN
65 - ATT'ALAAQ
66 - ATTAH'RIIM
67 - AL - MULK
68 - AL - QALAM
69 - AL - H'AAQQAH
70 - AL - MAA'RIJ
71 - NUH'
72 - AL - JINN
73 - AL - MUZZAMMIL
74 - AL - MUDDATHTHIR
75 - AL - QIYAMAH
76 - AL - INSAN
77 - AL - MURSALAAT
78 - ANNABAA
79 - ANNAZIA'AT
80 - A'BASA
81 - ATTAKWIR
82 - AL - INFIT'AAR
83 - AL - MUT'AFFIFIIN
84 - AL - INSHIQAAQ
85 - AL - BURUUJ
86 - ATT'AARIQ
87 - AL - AA'LAA
88 - AL - GHAASHIYAH
89 - AL - FAJR
90 - AL - BALAD
91 - ASH-SHAMS
92 - AL - LAYL
93 - WADH-DHUH'AA
94 - ASH-SHARH'
95 - AT-TIN
96 - AL - A'LAQ
97 - AL - QADR
98 - AL - BAYYINAH
99 - AZ-ZILZALAH
100 - AL - A'ADIYAAT
101 - AL - QAARIA'H
102 - AT-TAKAATHUR
103 - AL - A'S'R
104 - AL - HUMAZAH
105 - AL - FIIL
106 - QURAISH
107 - AL - MAAU'N
108 - AL - KAWTHAR
109 - AL - KAFIRUN
110 - ANNAS'R
111 - AL - MASAD
112 - AL - IKHLAS'
113 - AL - FALAQ
114 - ANNAS
KISWAHILI

38 - S'AAD

 

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 
1S'ad, Naapa kwa Qur'ani yenye mawaidha.
 
2Lakini walio kufuru wamo katika majivuno na upinzani
 
3Mataifa mangapi tumeyaangamiza kabla yao, na wakapiga kelele, lakini wakati wa kuokoka ulikwisha pita.
 
4Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anaye tokana nao wenyewe, na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo.
 
5Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu.
 
6Na wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia: Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu, kwani hili ni jambo lililo pangwa.
 
7Sisi hatukusikia haya katika mila hii ya mwisho. Haya si chochote ila ni uzushi tu.
 
8Ati yeye tu ndiye aliye teremshiwa mawaidha peke yake katika sisi? Lakini hao wana shaka na mawaidha yangu, bali hawajaionja adhabu yangu.
 
9Au wanazo wao khazina za rehema za Mola wako Mlezi, Mwenye nguvu, Mpaji?
 
10Au wao wana ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo kati yao? Basi nawazipande njia za kwendea huko!
 
11Hao ni askari watao shindwa miongoni mwa makundi yatayo shindwa.
 
12Walikanusha kabla yao kaumu ya Nuhu, na kina A'adi na Firauni mwenye majengo.
 
13Na Thamud na kaumu Lut'i na watu wa Machakani. Hayo ndiyo makundi.
 
14Hao wote waliwakadhibisha Mitume; basi wakastahiki adhabu yangu.
 
15Na hawa hawangojei ila ukelele mmoja tu usio na muda.
 
16Na wao husema: Mola wetu Mlezi! Tuletee upesi sehemu yetu ya adhabu kabla ya Siku ya Hisabu.
 
17Subiri kwa hayo wayasemayo, na umkumbuke mja wetu Daudi, mwenye nguvu. Hakika yeye alikuwa mwingi wa kutubia.
 
18Hakika tuliidhalilisha milima pamoja naye ikisabihi jioni na asubuhi pamoja naye.
 
19Na pia ndege walio kusanywa makundi kwa makundi; wote walikuwa wanyenyekevu kwake.
 
20Na tukautia nguvu ufalme wake, na tukampa hikima, na kukata hukumu.
 
21Na je! Imekufikia khabari ya wagombanao walipo pindukia ukuta kuingia chumbani?
 
22Walipo muingilia Daudi, naye akawaogopa. Wakasema: Usiogope! Sisi ni wagombanao wawili, mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe. Basi tuhukumu kwa haki, wala usipendelee. Na utuongoe kwenye njia iliyo sawa.
 
23Hakika huyu ndugu yangu ana kondoo wa kike tisiini na tisa; na mimi ninaye kondoo mke mmoja. Akasema: Nipe huyo nikufugie! Na amenishinda kwa maneno.
 
24Akasema: Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake. Na hakika washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipo kuwa walio amini na wakatenda mema. Na hao ni wachache. Na Daudi akajua kuwa tumemfanyia mtihani. Basi akamwomba msamaha Mola wake Mlezi, na akaanguka kusujudu na kutubia.
 
25Basi tukamsamehe kwa hayo. Naye kwa hakika anao mkaribisho mkubwa na marejeo mazuri kwetu.
 
26Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika wanao ipotea Njia ya Mwenyezi Mungu wakaiacha, watapata adhabu kali kwa sababu ya kusahau kwao Siku ya Hisabu.
 
27Na hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yao bure. Hiyo ni dhana ya walio kufuru. Ole wao walio kufuru kwa Moto utao wapata.
 
28Je! Tuwafanye walio amini na wakatenda mema kama wafanyao uharibifu katika nchi? Au tuwafanye wachamngu kama waovu?
 
29Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili.
 
30Na Daudi tukamtunukia Suleiman. Alikuwa mja mwema. Na hakika alikuwa mwingi wa kutubia.
 
31Alipo pelekewa jioni farasi wasimamao kidete, tayari kutoka shoti;
 
32Basi akasema: Navipenda vitu vizuri kwa kumkumbuka Mola wangu Mlezi. Kisha wakafichikana nyuma ya boma.
 
33(Akasema:) Nirudishieni! Akaanza kuwapapasa miguu na shingo.
 
34Na tulimtia mtihanini Suleiman, na tukauweka mwili juu ya kiti chake, kisha akarejea kwa kutubu.
 
35Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji.
 
36Basi tukaufanya upepo umtumikie, ukenda kwa amri yake, popote alipo taka kufika.
 
37Na tukayafanya mashet'ani yamtumikie, wote wajenzi na wapiga mbizi.
 
38Na wengine wafungwao kwa minyororo.
 
39Hichi ndicho kipawa chetu. Basi toa au zuia, bila ya hisabu.
 
40Na hakika yeye kwetu Sisi ana cheo cha kukaribishwa kwetu, na pahala pazuri pa kurejea.
 
41Na mkumbuke mja wetu Ayubu alipo mwita Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika Shet'ani amenifikishia udhia na adhabu.
 
42(Akaambiwa:) Piga-piga ardhi kwa mguu wako! Basi haya maji baridi ya kuogea na ya kunywa.
 
43Na tukampa ahali zake na wengine kama wao pamoja nao, kuwa ni rehema itokayo kwetu, na iwe kumbusho kwa watu wenye akili.
 
44Na shika kicha cha vijiti tu mkononi mwako, kisha ndio upigie nacho, wala usivunje kiapo. Hakika tulimkuta mwenye subira, mbora wa waja, kwa hakika alikuwa mwingi wa kutubu.
 
45Na wakumbuke waja wetu, Ibrahim na Is-haqa na Yaa'qubu walio kuwa na nguvu na busara.
 
46Sisi tumewakhusisha wao kwa sifa ya ukumbusho wa Akhera.
 
47Na hakika wao kwetu sisi ni wateuliwa walio bora.
 
48Na mkumbuke Ismail na Alyasaa na Dhulkifli, na wote hao ni katika walio bora.
 
49Huu ni ukumbusho. Na hakika wachamngu wana marudio mazuri.
 
50Bustani za milele zitazo funguliwa milango yao kwa ajili yao.
 
51Humo wataegemea matakia, wawe wanaagiza humo matunda mengi na vinywaji.
 
52Na pamoja nao wake zao wenye kutuliza macho, hirimu zao.
 
53Haya ndiyo mliyo ahidiwa kwa Siku ya Hisabu.
 
54Hakika hii ndiyo riziki yetu isiyo malizika.
 
55Ndio hivi! Na hakika wenye kuasi bila ya shaka watapata marudio maovu kabisa;
 
56Nayo ni Jahannamu! Wataingia humo. Nacho hicho ni kitanda kiovu mno cha kulalia.
 
57Ndio hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha!
 
58Na adhabu nyenginezo za namna hii.
 
59Hili ndilo kundi litakalo ingia pamoja nanyi. Hapana makaribisho mema kwao. Hakika hao wanaingia Motoni.
 
60Waseme: Lakini nyinyi! Hamna mapokezi mazuri! Nyinyi ndio mlio tusabibisha haya, napo ni pahala paovu kabisa!
 
61Waseme: Mola wetu Mlezi! Aliye tusabibisha haya mzidishie adhabu mara mbili Motoni.
 
62Watasema: Tuna nini hata hatuwaoni wale watu ambao tukiwahisabu ndio katika waovu?
 
63Tulikosea tulipo wafanyia maskhara, au macho yetu tu hayawaoni ?
 
64Hakika hayo bila ya shaka ndiyo makhasimiano ya watu wa Motoni.
 
65Sema: Hakika mimi ni mwonyaji tu; na hapana mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenda nguvu,
 
66Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na viliomo baina yake, Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe.
 
67Sema: Hii ni khabari kubwa kabisa.
 
68Ambayo nyinyi mnaipuuza.
 
69Sikuwa na ilimu ya mambo ya viumbe wakuu watukufu walipo kuwa wakishindana.
 
70Haikufunuliwa kwangu isipo kuwa ya kwamba hakika mimi ni mwonyaji dhaahiri.
 
71Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo.
 
72Na nitakapo mkamilisha na kumpulizia roho inayo tokana nami, basi muangukieni kwa kumt'ii.
 
73Basi Malaika wakat'ii wote pamoja.
 
74Isipo kuwa Iblisi; alijivuna na akawa katika makafiri.
 
75Mwenyezi Mungu akamwambia: Ewe Iblisi! Kipi kilicho kuzuia kumt'ii yule niliye muumba kwa mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu kweli?
 
76Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo.
 
77Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika.
 
78Na hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo.
 
79Akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watayo fufuliwa viumbe.
 
80Mwenyezi Mungu akasema: Basi umekwisha kuwa miongoni mwa walio pewa muhula,
 
81Mpaka siku ya wakati maalumu.
 
82Akasema (Iblisi): Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote,
 
83Isipo kuwa wale waja wako miongoni mwao walio khitariwa.
 
84Akasema: Haki! Na haki ninaisema.
 
85Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wewe na kwa hao wote wenye kukufuata miongoni mwao.
 
86Sema (Ewe Mtume) : Sikuombeni ujira juu ya haya, wala mimi si katika wadanganyifu.
 
87Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote.
 
88Na bila ya shaka mtajua khabari zake baada ya muda.