99 - AZ-ZILZALAH |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake! |
|
2 | Na itakapo toa ardhi mizigo yake! |
|
3 | Na mtu akasema: Ina nini? |
|
4 | Siku hiyo itahadithia khabari zake. |
|
5 | Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia! |
|
6 | Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao! |
|
7 | Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona! |
|
8 | Na anaye tenda chembe ya uovu atauona! |
|