100 - AL - A'ADIYAAT |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua, |
|
2 | Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini, |
|
3 | Wakishambulia wakati wa asubuhi, |
|
4 | Huku wakitimua vumbi, |
|
5 | Na wakijitoma kati ya kundi, |
|
6 | Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi! |
|
7 | Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo! |
|
8 | Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali! |
|
9 | Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini? |
|
10 | Na yakakusanywa yaliomo vifuani? |
|
11 | Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote! |
|