68 - AL - QALAM |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Nuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo, |
|
2 | Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu. |
|
3 | Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika. |
|
4 | Na hakika wewe una tabia tukufu. |
|
5 | Karibu utaona, na wao wataona, |
|
6 | Ni nani kati yenu aliye pandwa na wazimu. |
|
7 | Hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye ajuaye zaidi nani aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka. |
|
8 | Basi usiwat'ii wanao kadhibisha. |
|
9 | Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie. |
|
10 | Wala usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa, |
|
11 | Mtapitapi, apitaye akifitini, |
|
12 | Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi, |
|
13 | Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu. |
|
14 | Ati kwa kuwa ana mali na watoto! |
|
15 | Anapo somewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za uwongo za watu wa zamani! |
|
16 | Tutamtia kovu juu ya pua yake. |
|
17 | Hakika tumewajaribu hawa kama tulivyo wajaribu wale wenye shamba, walipo apa kwamba watayavuna mazao yake itakapo kuwa asubuhi. |
|
18 | Wala hawakusema: Mungu akipenda! |
|
19 | Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako Mlezi, nao wamelala! |
|
20 | Likawa kama usiku wa giza. |
|
21 | Asubuhi wakaitana. |
|
22 | Ya kwamba nendeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna. |
|
23 | Basi walikwenda na huku wakinong'onezana, |
|
24 | Ya kuwa leo hata masikini mmoja asikuingilieni. |
|
25 | Na walikwenda asubuhi, nao wameshikilia azimio hilo. |
|
26 | Basi walipo liona, wakasema: Hakika tumepotea! |
|
27 | Bali tumenyimwa! |
|
28 | Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu? |
|
29 | Wakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu. |
|
30 | Basi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao. |
|
31 | Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka! |
|
32 | Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. |
|
33 | Namna hivi yanakuwa mateso, na bila ya shaka mateso ya Akhera ni makubwa zaidi, laiti wangeli jua! |
|
34 | Hakika wachamngu watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao Mlezi. |
|
35 | Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu? |
|
36 | Mna nini? Mnahukumu vipi? |
|
37 | Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma? |
|
38 | Kuwa mtapata humo mnayo yapenda? |
|
39 | Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika mtapata kila mnayo jihukumia? |
|
40 | Waulize: Ni nani miongoni mwao dhamini wa haya? |
|
41 | Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanasema kweli. |
|
42 | Siku utakapo wekwa wazi mundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza, |
|
43 | Macho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipo kuwa wazima - |
|
44 | Basi niache na wanao kadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kwa mahali wasipo pajua. |
|
45 | Na ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni imara. |
|
46 | Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo? |
|
47 | Au iko kwao siri, basi wao wanaiandika? |
|
48 | Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe kama mmezwa na samaki, alipo nadi naye kazongwa. |
|
49 | Kama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa. |
|
50 | Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema. |
|
51 | Na walio kufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanapo sikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu. |
|
52 | Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. |
|