95 - AT-TIN |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Naapa kwa tini na zaituni! |
|
2 | Na kwa Mlima wa Sinai! |
|
3 | Na kwa mji huu wenye amani! |
|
4 | Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa. |
|
5 | Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini! |
|
6 | Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha. |
|
7 | Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo? |
|
8 | Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote? |
|