56 - AL -WAAQIA'H |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Litakapo tukia hilo Tukio |
|
2 | Hapana cha kukanusha kutukia kwake. |
|
3 | Literemshalo linyanyualo, |
|
4 | Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso, |
|
5 | Na milima itapo sagwasagwa, |
|
6 | Iwe mavumbi yanayo peperushwa, |
|
7 | Na nyinyi mtakuwa namna tatu:- |
|
8 | Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani? |
|
9 | Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni? |
|
10 | Na wa mbele watakuwa mbele. |
|
11 | Hao ndio watakao karibishwa |
|
12 | Katika Bustani zenye neema. |
|
13 | Fungu kubwa katika wa mwanzo, |
|
14 | Na wachache katika wa mwisho. |
|
15 | Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa. |
|
16 | Wakiviegemea wakielekeana. |
|
17 | Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele, |
|
18 | Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi. |
|
19 | Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa. |
|
20 | Na matunda wayapendayo, |
|
21 | Na nyama za ndege kama wanavyo tamani. |
|
22 | Na Mahurulaini, |
|
23 | Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa. |
|
24 | Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda. |
|
25 | Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi, |
|
26 | Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama. |
|
27 | Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani? |
|
28 | Katika mikunazi isiyo na miba, |
|
29 | Na migomba iliyo pangiliwa, |
|
30 | Na kivuli kilicho tanda, |
|
31 | Na maji yanayo miminika, |
|
32 | Na matunda mengi, |
|
33 | Hayatindikii wala hayakatazwi, |
|
34 | Na matandiko yaliyo nyanyuliwa. |
|
35 | Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya, |
|
36 | Na tutawafanya vijana, |
|
37 | Wanapendana na waume zao, hirimu moja. |
|
38 | Kwa ajili ya watu wa kuliani. |
|
39 | Fungu kubwa katika wa mwanzo, |
|
40 | Na fungu kubwa katika wa mwisho. 3 |
|
41 | Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni? |
|
42 | Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka, |
|
43 | Na kivuli cha moshi mweusi, |
|
44 | Si cha kuburudisha wala kustarehesha. |
|
45 | Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa. |
|
46 | Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa, |
|
47 | Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa? |
|
48 | Au baba zetu wa zamani? |
|
49 | Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho |
|
50 | Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu. |
|
51 | Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha, |
|
52 | Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu. |
|
53 | Na kwa mti huo mtajaza matumbo. |
|
54 | Na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka. |
|
55 | Tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu. |
|
56 | Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo. |
|
57 | Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki? |
|
58 | Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza? |
|
59 | Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji? |
|
60 | Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi |
|
61 | Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua. |
|
62 | Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki? |
|
63 | Je! Mnaona makulima mnayo yapanda? |
|
64 | Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha? |
|
65 | Tungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu, |
|
66 | Mkisema: Hakika sisi tumegharimika; |
|
67 | Bali sisi tumenyimwa. |
|
68 | Je! Mnayaona maji mnayo yanywa? |
|
69 | Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha? |
|
70 | Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru? |
|
71 | Je! Mnauona moto mnao uwasha? |
|
72 | Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji? |
|
73 | Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani. |
|
74 | Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu. |
|
75 | Basi naapa kwa maanguko ya nyota, |
|
76 | Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua! |
|
77 | Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu, |
|
78 | Katika Kitabu kilicho hifadhiwa. |
|
79 | Hapana akigusaye ila walio takaswa. |
|
80 | Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
|
81 | Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza? |
|
82 | Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha? |
|
83 | Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo, |
|
84 | Na nyinyi wakati huo mnatazama! |
|
85 | Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi. |
|
86 | Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu, |
|
87 | Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli? |
|
88 | Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa, |
|
89 | Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema. |
|
90 | Na akiwa katika watu wa upande wa kulia, |
|
91 | Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia. |
|
92 | Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu, |
|
93 | Basi karamu yake ni maji yanayo chemka, |
|
94 | Na kutiwa Motoni. |
|
95 | Hakika hii ndiyo haki yenye yakini. |
|
96 | Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa. |
|