86 - ATT'AARIQ |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku! |
|
2 | Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku? |
|
3 | Ni Nyota yenye mwanga mkali. |
|
4 | Hapana nafsi ila inayo mwangalizi. |
|
5 | Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani? |
|
6 | Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa, |
|
7 | Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu. |
|
8 | Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha. |
|
9 | Siku zitakapo dhihirishwa siri. |
|
10 | Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi. |
|
11 | Naapa kwa mbingu yenye marejeo! |
|
12 | Na kwa ardhi inayo pasuka! |
|
13 | Hakika hii ni kauli ya kupambanua. |
|
14 | Wala si mzaha. |
|
15 | Hakika wao wanapanga mpango. |
|
16 | Na Mimi napanga mpango. |
|
17 | Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole. |
|