81 - ATTAKWIR |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Jua litakapo kunjwa, s |
|
2 | Na nyota zikazimwa, |
|
3 | Na milima ikaondolewa, |
|
4 | Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe, |
|
5 | Na wanyama wa mwituni wakakusanywa, |
|
6 | Na bahari zikawaka moto, |
|
7 | Na nafsi zikaunganishwa, |
|
8 | Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa, |
|
9 | Kwa kosa gani aliuliwa? |
|
10 | Na madaftari yatakapo enezwa, |
|
11 | Na mbingu itapo tanduliwa, |
|
12 | Na Jahannamu itapo chochewa, |
|
13 | Na Pepo ikasogezwa, |
|
14 | Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha. |
|
15 | Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma, |
|
16 | Zinazo kwenda, kisha zikajificha, |
|
17 | Na kwa usiku unapo pungua, |
|
18 | Na kwa asubuhi inapo pambazuka, |
|
19 | Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu, |
|
20 | Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi, |
|
21 | Anaye t'iiwa, tena muaminifu. |
|
22 | Na wala huyu mwenzenu hana wazimu. |
|
23 | Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi. |
|
24 | Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu. |
|
25 | Wala hii si kauli ya Shetani maluuni. |
|
26 | Basi mnakwenda wapi? |
|
27 | Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. |
|
28 | Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa. |
|
29 | Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote. |
|