70 - AL - MAA'RIJ |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea, |
|
2 | Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia - |
|
3 | Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja. |
|
4 | Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu! |
|
5 | Basi subiri kwa subira njema. |
|
6 | Hakika wao wanaiona iko mbali, |
|
7 | Na Sisi tunaiona iko karibu. |
|
8 | Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa. |
|
9 | Na milima itakuwa kama sufi. |
|
10 | Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake. |
|
11 | Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe, |
|
12 | Na mkewe, na nduguye, |
|
13 | Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu, |
|
14 | Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye. |
|
15 | La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa, |
|
16 | Unao babua ngozi ya kichwa! |
|
17 | Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka. |
|
18 | Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi. |
|
19 | Hakika mtu ameumbwa na papara. |
|
20 | Inapo mgusa shari hupapatika. |
|
21 | Na inapo mgusa kheri huizuilia. |
|
22 | Isipo kuwa wanao sali, |
|
23 | Ambao wanadumisha Sala zao, |
|
24 | Na ambao katika mali yao iko haki maalumu |
|
25 | Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba; |
|
26 | Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo, |
|
27 | Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi. |
|
28 | Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo. |
|
29 | Na ambao wanahifadhi tupu zao. |
|
30 | Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi - |
|
31 | Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka. |
|
32 | Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao, |
|
33 | Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao, |
|
34 | Na ambao wanazihifadhi Sala zao. |
|
35 | Hao ndio watakao hishimiwa Peponi. |
|
36 | Wana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho tu? |
|
37 | Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto! |
|
38 | Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema? |
|
39 | La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua. |
|
40 | Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza |
|
41 | Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi. |
|
42 | Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa, |
|
43 | Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo, |
|
44 | Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyo kuwa wakiahidiwa. |
|