105 - AL - FIIL |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo? |
|
2 | Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika? |
|
3 | Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi, |
|
4 | Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni, |
|
5 | Akawafanya kama majani yaliyo liwa! |
|