___Translations___

_Quran?_

_Gadgets_

_Search_

_Links_

_Contribute_

_Note_

1 - AL-FAATIH'A
2 - AL - BAQARA
3 - AL I'MRAN
4 - AN-NISAAI
5 - AL - MAIDA
6 - AL - AN-A'AM
7 - AL - A'RAAF
8 - AL - ANFAAL
9 - AT-TAWBA
10 - YUNUS
11 - HUD
12 - YUSUF
13 - AR-RAA'D
14 - IBRAHIM
15 - AL - HIJR
16 - AN NAH'L
17 - AL ISRAAI (BANI ISRAIL)
18 - AL - KAHF
19 - MARYAM
20 - T'AHA
21 - AL - ANBIYAA
22 - AL -HAJJ
23 - AL - MUUMINUN
24 - AN - NUR
25 - AL - FURQAN
26 - ASH-SHUA'RAA
27 - AN-NAML
28 - AL-QAS'AS'
29 - AL - A'NKABUT
30 - AR-RUM
31 - LUQMAN
32 - ASSAJDAH
33 - AL-AH'ZAB
34 - SABAA
35 - FAAT'IR
36 - YA-SIN
37 - ASS'AFFAT
38 - S'AAD
39 - AZZUMAR
40 - GHAAFIR (AU AL MUUMIN)
41 - FUSS'ILAT (AU H'A MIM SAJDAH)
42 - ASH-SHUURA
43 - AZZUKHRUF
44 - ADDUKHAN
45 - AL - JAATHIYA
46 - AL - AH'QAAF
47 - MUH'AMMAD
48 - AL FAT-H'I
49 - AL H'UJURAAT
50 - QAAF
51 - ADH-DHAARIYAAT
52 - ATT'UR
53 - ANNAJM
54 - AL-QAMAR
55 - ARRAH'MAN
56 - AL -WAAQIA'H
57 - AL -H'ADIID
58 - AL - MUJAADALAH
59 - AL - H'ASHRI
60 - AL - MUMTAH'INAH
61 - ASS'AF
62 - AL - JUMUA'
63 - AL - MUNAAFIQUN
64 - ATTAGHAABUN
65 - ATT'ALAAQ
66 - ATTAH'RIIM
67 - AL - MULK
68 - AL - QALAM
69 - AL - H'AAQQAH
70 - AL - MAA'RIJ
71 - NUH'
72 - AL - JINN
73 - AL - MUZZAMMIL
74 - AL - MUDDATHTHIR
75 - AL - QIYAMAH
76 - AL - INSAN
77 - AL - MURSALAAT
78 - ANNABAA
79 - ANNAZIA'AT
80 - A'BASA
81 - ATTAKWIR
82 - AL - INFIT'AAR
83 - AL - MUT'AFFIFIIN
84 - AL - INSHIQAAQ
85 - AL - BURUUJ
86 - ATT'AARIQ
87 - AL - AA'LAA
88 - AL - GHAASHIYAH
89 - AL - FAJR
90 - AL - BALAD
91 - ASH-SHAMS
92 - AL - LAYL
93 - WADH-DHUH'AA
94 - ASH-SHARH'
95 - AT-TIN
96 - AL - A'LAQ
97 - AL - QADR
98 - AL - BAYYINAH
99 - AZ-ZILZALAH
100 - AL - A'ADIYAAT
101 - AL - QAARIA'H
102 - AT-TAKAATHUR
103 - AL - A'S'R
104 - AL - HUMAZAH
105 - AL - FIIL
106 - QURAISH
107 - AL - MAAU'N
108 - AL - KAWTHAR
109 - AL - KAFIRUN
110 - ANNAS'R
111 - AL - MASAD
112 - AL - IKHLAS'
113 - AL - FALAQ
114 - ANNAS
KISWAHILI

15 - AL - HIJR

 

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 
1Alif Lam Ra. (A.L.R). Hizi ni Aya za Kitabu na Qur'ani inayo bainisha.
 
2HUENDA ikawa walio kufuru wakatamani wange kuwa Waislamu.
 
3Waache wale, na wastarehe, na iwazuge tamaa. Watakuja jua.
 
4Na hatukuuangamiza mji wowote ule ila ulikuwa na muda wake maalumu.
 
5Hawawezi watu wowote kuitangulia ajali yao, wala kuchelewa.
 
6Na walisema: Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu.
 
7Mbona hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli?
 
8Sisi hatuwateremshi Malaika ila kwa sababu ya haki, na hapo hawatapewa muhula.
 
9Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.
 
10Na hakika tulikwisha watumia Mitume mataifa ya mwanzo.
 
11Na hakuwafikia Mtume ila walimkejeli.
 
12Na kama hivi ndivyo tunavyo ingiza katika nyoyo za wakosefu.
 
13Hawayaamini haya, na hali ya kuwa umekwisha wapitia mfano wa watu wa kale.
 
14Na lau tungeli wafungulia mlango wa mbingu, wakawa wanapanda,
 
15Basi wangeli sema: Macho yetu yamelevywa, bali sisi wenyewe tumerogwa.
 
16Na hakika tumeweka katika mbingu vituo vya sayari, na tumezipamba kwa wenye kuangalia.
 
17Na tumezilinda na kila shetani afukuzwaye.
 
18Isipo kuwa mwenye kusikiliza kwa kuibia, naye hufuatwa na kijinga cha moto kinacho onekana.
 
19Na ardhi tumeitandaza na humo tumeweka milima, na tumeotesha kila kitu kwa kiasi chake.
 
20Na tumekujaalieni humo vitu vya maisha yenu, na ya hao ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku.
 
21Na hakuna chochote ila asili yake inatokana na Sisi; wala hatukiteremshi ila kwa kipimo maalumu.
 
22Na tunazipeleka pepo za kupandishia, na tunateremsha kutoka mbinguni maji, kisha tukakunywesheni maji hayo. Wala si nyinyi mnayo yaweka.
 
23Na Sisi ndio tunao huisha na tunao fisha. Na Sisi ndio Warithi.
 
24Na tunawajua walio tangulia katika nyinyi, na tunawajua walio taakhari.
 
25Na hakika Mola wako Mlezi ndiye atakaye wakusanya. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mjuzi.
 
26Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.
 
27Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto.
 
28Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.
 
29Basi nitakapo mkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi mumwangukie kumsujudia.
 
30Basi Malaika wote pamoja walimsujudia,
 
31Isipo kuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na walio sujudu.
 
32(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Iblisi! Una nini hata hukuwa pamoja na walio sujudu?
 
33Akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliye muumba kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yenye sura.
 
34(Mwenyezi Mungu) akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe ni maluuni!
 
35Na hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo.
 
36Akasema (Iblisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watapo fufuliwa.
 
37(Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika walio pewa muhula
 
38Mpaka siku ya wakati maalumu.
 
39Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote,
 
40Ila waja wako walio safika.
 
41Akasema: Hii Njia ya kujia kwangu Iliyo Nyooka.
 
42Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipo kuwa wale wapotofu walio kufuata.
 
43Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipo ahidiwa wote.
 
44Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio tengewa.
 
45Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem.
 
46(Wataambiwa:) Ingieni kwa salama na amani.
 
47Na tutaondoa chuki iliyo kuwamo vifuani mwao, wawe ndugu juu ya viti vya enzi wameelekeana.
 
48Humo hayatawagusa machofu, wala hawatatolewa humo.
 
49Waambie waja wangu ya kwamba Mimi ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
 
50Na kwamba adhabu yangu ndio adhabu iliyo chungu!
 
51Na uwape khabari za wageni wa Ibrahim.
 
52Walipo ingia kwake na wakasema: Salama! Yeye akasema: Hakika sisi tunakuogopeni.
 
53Wakasema: Usiogope. Sisi tunakubashiria kijana mwenye ujuzi.
 
54Akasema: Mnanibashiria nami uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanibashiria?
 
55Wakasema: Tunakubashiria kwa haki; basi usiwe miongoni mwa wanao kata tamaa.
 
56Akasema: Na nani anaye kata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi ila wale walio potea?
 
57Akasema: Hebu nini amri yenu, enyi wajumbe?
 
58Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya wakosefu!
 
59Isipo kuwa walio mfuata Luut'i. Bila ya shaka sisi tutawaokoa hao wote.
 
60Ila mkewe. Tunakadiria huyo atakuwa miongoni watao bakia nyuma.
 
61Basi wale wajumbe walipo fika kwa Luut'i,
 
62Alisema (Luut'i): Hakika nyinyi ni watu msio juulikana.
 
63Wakasema: Bali sisi tumekuletea yale waliyo kuwa wakiyafanyia shaka.
 
64Na tumefika kwako kwa Haki, na hakika sisi tunasema kweli.
 
65Basi ondoka na ahli zako usiku ungalipo, nawe ufuate nyuma yao, wala yeyote kati yenu asigeuke nyuma. Na mwende mnapo amrishwa.
 
66Na tukamfunulia hukumu hiyo, ya kwamba hata wa mwisho wao hao ikifika asubuhi atakuwa kesha katiliwa mbali.
 
67Na wakaja watu wa mji ule nao furahani.
 
68Akasema: Hakika hawa wageni wangu, basi msinifedheheshe.
 
69Na mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi.
 
70Wakasema: Sisi hatukukukataza usimkaribishe yeyote?
 
71Akasema: Hawa binti zangu, ikiwa nyinyi ni watendaji.
 
72Naapa kwa umri wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo.
 
73Ukelele ukawatwaa wakipambaukiwa.
 
74Na tukaigeuza nchi juu chini, na tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo wa Motoni.
 
75Hakika katika hayo zipo ishara kwa waaguzi.
 
76Na miji hii ipo kwenye njia inayo pitiwa.
 
77Hakika katika hayo ipo ishara kwa Waumini.
 
78Na hakika watu wa Kichakani walikuwa wenye kudhulumu.
 
79Kwa hivyo tukawaadhibu. Na nchi mbili hizi ziko kwenye njia ilio wazi.
 
80Na bila ya shaka wakaazi wa Hijr waliwakanusha Mitume.
 
81Na tuliwapa ishara zetu, nao wakazipuuza.
 
82Nao walikuwa wakichonga majumba katika milima kwa amani.
 
83Basi ukelele ukawatwaa asubuhi.
 
84Hayakuwafaa waliyo kuwa wakiyachuma.
 
85Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ila kwa ajili ya Haki. Na hakika Kiyama kitafika. Basi samehe msamaha mzuri.
 
86Hakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji Mjuzi.
 
87Na tumekupa Aya saba zinazo somwa mara kwa mara, na Qur'ani Tukufu.
 
88Usivitumbulie macho yako vitu tulivyo waneemesha makundi fulani kati yao, wala usiwahuzunikie. Na wainamishie bawa lako (la huruma) Waumini.
 
89Na sema: Hakika mimi ni mwonyaji mwenye kubainisha.
 
90Kama hivyo tuliwateremshia walio gawa,
 
91Ambao wakaifanya Qur'ani vipande vipande.
 
92Basi Naapa kwa Mola wako Mlezi! Tutawahoji wote,
 
93Kwa waliyo kuwa wakiyatenda.
 
94Basi wewe yatangaze uliyo amrishwa, na jitenge na washirikina.
 
95Hakika Sisi tunatosha kukukinga na wanao kejeli.
 
96Hao wanao fanya kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu yupo mungu mwingine. Basi, watakuja jua!
 
97Na Sisi tunajua kwa hakika kuwa wewe kifua chako kinaona dhiki kwa hayo wayasemayo.
 
98Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni wanao msujudia.
 
99Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini.