___Translations___

_Quran?_

_Gadgets_

_Search_

_Links_

_Contribute_

_Note_

1 - AL-FAATIH'A
2 - AL - BAQARA
3 - AL I'MRAN
4 - AN-NISAAI
5 - AL - MAIDA
6 - AL - AN-A'AM
7 - AL - A'RAAF
8 - AL - ANFAAL
9 - AT-TAWBA
10 - YUNUS
11 - HUD
12 - YUSUF
13 - AR-RAA'D
14 - IBRAHIM
15 - AL - HIJR
16 - AN NAH'L
17 - AL ISRAAI (BANI ISRAIL)
18 - AL - KAHF
19 - MARYAM
20 - T'AHA
21 - AL - ANBIYAA
22 - AL -HAJJ
23 - AL - MUUMINUN
24 - AN - NUR
25 - AL - FURQAN
26 - ASH-SHUA'RAA
27 - AN-NAML
28 - AL-QAS'AS'
29 - AL - A'NKABUT
30 - AR-RUM
31 - LUQMAN
32 - ASSAJDAH
33 - AL-AH'ZAB
34 - SABAA
35 - FAAT'IR
36 - YA-SIN
37 - ASS'AFFAT
38 - S'AAD
39 - AZZUMAR
40 - GHAAFIR (AU AL MUUMIN)
41 - FUSS'ILAT (AU H'A MIM SAJDAH)
42 - ASH-SHUURA
43 - AZZUKHRUF
44 - ADDUKHAN
45 - AL - JAATHIYA
46 - AL - AH'QAAF
47 - MUH'AMMAD
48 - AL FAT-H'I
49 - AL H'UJURAAT
50 - QAAF
51 - ADH-DHAARIYAAT
52 - ATT'UR
53 - ANNAJM
54 - AL-QAMAR
55 - ARRAH'MAN
56 - AL -WAAQIA'H
57 - AL -H'ADIID
58 - AL - MUJAADALAH
59 - AL - H'ASHRI
60 - AL - MUMTAH'INAH
61 - ASS'AF
62 - AL - JUMUA'
63 - AL - MUNAAFIQUN
64 - ATTAGHAABUN
65 - ATT'ALAAQ
66 - ATTAH'RIIM
67 - AL - MULK
68 - AL - QALAM
69 - AL - H'AAQQAH
70 - AL - MAA'RIJ
71 - NUH'
72 - AL - JINN
73 - AL - MUZZAMMIL
74 - AL - MUDDATHTHIR
75 - AL - QIYAMAH
76 - AL - INSAN
77 - AL - MURSALAAT
78 - ANNABAA
79 - ANNAZIA'AT
80 - A'BASA
81 - ATTAKWIR
82 - AL - INFIT'AAR
83 - AL - MUT'AFFIFIIN
84 - AL - INSHIQAAQ
85 - AL - BURUUJ
86 - ATT'AARIQ
87 - AL - AA'LAA
88 - AL - GHAASHIYAH
89 - AL - FAJR
90 - AL - BALAD
91 - ASH-SHAMS
92 - AL - LAYL
93 - WADH-DHUH'AA
94 - ASH-SHARH'
95 - AT-TIN
96 - AL - A'LAQ
97 - AL - QADR
98 - AL - BAYYINAH
99 - AZ-ZILZALAH
100 - AL - A'ADIYAAT
101 - AL - QAARIA'H
102 - AT-TAKAATHUR
103 - AL - A'S'R
104 - AL - HUMAZAH
105 - AL - FIIL
106 - QURAISH
107 - AL - MAAU'N
108 - AL - KAWTHAR
109 - AL - KAFIRUN
110 - ANNAS'R
111 - AL - MASAD
112 - AL - IKHLAS'
113 - AL - FALAQ
114 - ANNAS
KISWAHILI

13 - AR-RAA'D

 

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

 
1Alif Lam Mym Ra. (A.L.M.R.) Hizi ni Ishara za Kitabu. Na uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki. Lakini wengi wa watu hawaamini.
 
2Mwenyezi Mungu aliye ziinua mbingu bila ya nguzo mnazo ziona, ametawala kwenye Ufalme wake, na amefanya jua na mwezi yamt'ii, kila kimoja kinakwenda kwa kiwango maalumu. Anayapanga mambo, na anazipambanua Ishara ili mpate kuwa na yakini kukutana na Mola wenu Mlezi.
 
3Na ndiye aliye itandaza ardhi na akaweka humo milima na mito. Na katika kila matunda akafanya dume na jike. Huufunika usiku juu ya mchana. Hakika katika haya zimo Ishara kwa watu wanao fikiri.
 
4Na katika ardhi vimo vipande vilivyo karibiana, na zipo bustani za mizabibu, na mimea mingine, na mitende yenye kuchipua kwenye shina moja na isio chipua kwenye shina moja, nayo inatiliwa maji yale yale. Na tunaifanya baadhi yao bora kuliko mengine katika kula. Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanao tia mambo akilini.
 
5Na kama ukistaajabu, basi cha ajabu zaidi ni huo usemi wao: Ati tukisha kuwa mchanga kweli tutakuwa katika umbo jipya? Hao ndio walio mkufuru Mola wao Mlezi. Na hao ndio watao kuwa na makongwa shingoni mwao, na hao ndio watu wa Motoni. Humo watadumu.
 
6Na wanakuhimiza ulete maovu kabla ya mema, hali ya kuwa zimekwisha pita kabla yao adhabu za kupigiwa mfano. Na hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye msamaha kwa watu juu ya udhalimu wao. Na hakika Mola wako Mlezi ni Mkali wa kuadhibu.
 
7Na wale walio kufuru husema: Mbona hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi? Hakika wewe ni Mwonyaji, na kila kaumu ina wa kuwaongoa.
 
8Mwenyezi Mungu anajua mimba abebayo kila mwanamke, na kinacho punguka na kuzidi matumboni. Na kila kitu kwake ni kwa kipimo.
 
9Yeye ndiye Mwenye kujua yanayo onekana na yasio onekana; Mkuu Aliye tukuka.
 
10Ni sawa anaye ficha kauli yake kati yenu na anaye idhihirisha, na anaye jibanza usiku na anaye tembea jahara mchana.
 
11Kila mtu analo kundi la malaika mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao. Na Mwenyezi Mungu anapo watakia watu adhabu hakuna cha kuzuia wala hawana mlinzi yeyote badala yake.
 
12Yeye ndiye anaye kuonyesheni umeme kwa khofu na tamaa, na huyaleta mawingu mazito.
 
13Na radi inamtakasa Mwenyezi Mungu kwa kumhimidi, na Malaika pia, kwa kumkhofu. Naye hupeleka mapigo ya radi yakampata amtakaye. Nao wanabishana juu ya Mwenyezi Mungu. Na Yeye ni Mwenye adhabu kali!
 
14Wa kuombwa kweli ni Yeye tu. Na hao wanao waomba badala yake hawawajibu chochote; bali ni kama mwenye kunyoosha viganja vyake kwenye maji ili yafike kinywani mwake, lakini hayafiki. Na maombi ya makafiri hayako ila katika upotovu.
 
15Na viliomo mbinguni na katika ardhi vinamsujudia Mwenyezi Mungu tu vikitaka visitake. Na pia vivuli vyao asubuhi na jioni.
 
16Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu na ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, mnawafanya wenginewe badala yake kuwa ni walinzi, nao hawajifai wenyewe kwa jema wala baya? Sema: Hebu kipofu na mwenye kuona huwa sawa? Au hebu huwa sawa giza na mwangaza? Au wamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika walio umba kama alivyo umba Yeye, na viumbe hivyo vikawadanganyikia? Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda!
 
17Ameteremsha maji kutoka mbinguni. Na mabonde yakamiminika maji kwa kadiri yake. Na mafuriko yakachukua mapovu yaliyo kusanyika juu yake. Na kutokana na wanavyo yayusha katika moto kwa kutaka mapambo au vyombo hutokea povu vile vile. Namna hivyo Mwenyezi Mungu ndivyo anavyo piga mifano ya Haki na baat'ili. Basi lile povu linapita kama takataka tu basi. Ama kinacho wafaa watu hubakia kwenye ardhi. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo piga mifano.
 
18Walio muitikia Mola wao Mlezi watapata wema. Na wasio muitikia, hata wangeli kuwa navyo vyote viliomo katika ardhi na mfano wa hivyo, bila ya shaka wangeli vitoa kujikombolea! Hao watapata hisabu mbaya kabisa, na makao yao ni Jahannamu. Na hapo ni pahala pabaya mno!
 
19Je! Anaye jua ya kwamba yaliyo teremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki ni sawa na aliye kipofu? Wenye akili ndio wanao zingatia,
 
20Wale ambao wanatimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu, wala hawavunji maagano.
 
21Na wale ambao huyaunga aliyo amrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanaikhofu hisabu mbaya.
 
22Na ambao husubiri kwa kutaka radhi ya Mola wao Mlezi, na wakashika Sala, na wakatoa, kwa siri na kwa uwazi, katika tulivyo wapa; na wakayaondoa maovu kwa wema. Hao ndio watakao pata malipo ya Nyumba ya Akhera.
 
23Nayo ni Bustani za milele, wataziingia wao na walio wema miongoni mwa baba zao, na wake zao, na vizazi vyao. Na Malaika wanawaingilia katika kila mlango.
 
24(Wakiwaambia) Assalamu Alaikum! Amani iwe juu yenu, kwa sababu ya mlivyo subiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera.
 
25Na wale wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kuzifunga, na wanakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanafanya fisadi katika nchi: hao ndio watakao pata laana, na watapata Nyumba mbaya.
 
26Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye, na humkunjia kwa kipimo. Na wamefurahia maisha ya dunia. Na uhai wa dunia kwa kulingana na Akhera si kitu ila ni starehe ndogo.
 
27Na wanasema walio kufuru: Kwa nini hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi. Sema: Hakika Mwenyezi Mungu humwacha kupotea amtakaye, na humwongoa anaye elekea kwake,
 
28Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua!
 
29Wale walio amini na wakatenda mema watakuwa na raha na marejeo mazuri.
 
30Ndio kama hivi tumekutuma kwa umma ambao wamekwsiha pita kabla yao umati nyengine, ili uwasomee tunayo kufunulia, na wao wanamkufuru Rahmani, Mwingi wa Rehema! Sema: Yeye ndiye Mola wangu Mlezi. Hapana mungu isipo kuwa Yeye. Juu yake nimetegemea, na kwake ndio marejeo yangu!
 
31Na kama ingeli kuwako Qur'ani ndiyo inayo endeshewa milima, na kupasuliwa ardhi, na kusemeshewa wafu, (basi ingeli kuwa Qur'ani hii). Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Je, hawajajua walio amini kwamba lau kuwa Mwenyezi Mungu ange penda bila ya shaka angeli waongoa watu wote? Wala walio kufuru hawaachi kusibiwa na balaa kwa waliyo yatenda, au ikawateremkia karibu na nyumbani kwao, mpaka ifike ahadi ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake.
 
32Na hakika walifanyiwa kejeli Mitume walio kuwa kabla yako. Na nikawapururia wale walio kufuru, kisha nikawashika! Basi ilikuwaje adhabu yangu!
 
33Je! Anaye isimamia kila nafsi kwa yale iliyo yachuma...? Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu kuwa na washirika! Sema watajeni. Au ndio mnampa khabari ya yale asiyo yajua katika ardhi; au ni maneno matupu? Bali walio kufuru wamepambiwa vitimbi vyao na wamezuiliwa njia. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha apotee basi hana wa kumwongoa.
 
34Wanayo adhabu katika maisha ya dunia, na adhabu ya Akhera hapana shaka ina mashaka zaidi. Na wala hawatakuwa na wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu.
 
35Mfano wa Bustani waliyo ahidiwa wachamngu, kati yake inapita mito, matunda yake ni ya daima, na pia kivuli chake. Huu ndio mwisho wa wale walio walio jilinda. Na mwisho wa makafiri ni Moto.
 
36Na tulio wapa Kitabu wanafurahia uliyo teremshiwa. Na katika makundi mengine wapo wanao yakataa baadhi ya haya. Sema: Nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu, na wala nisimshirikishe. Kuendea kwake Yeye ndiyo ninaita, na kwake Yeye ndio marejeo yangu.
 
37Na ndio kama hivi tumeiteremsha Qur'ani kuwa ni hukumu kwa lugha ya Kiarabu. Na ukifuata matamanio yao baada ya kukujia ilimu hii, hutakuwa na rafiki wala mlinzi mbele ya Mwenyezi Mungu.
 
38Na hakika Sisi tulikwisha watuma Mitume kabla yako, na tukajaalia wawe na wake na dhuriya. Na haiwi kwa Mtume kuleta miujiza isipo kuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kila kipindi kina hukumu yake.
 
39Mwenyezi Mungu hufuta na huthibitisha ayatakayo. Na asili ya hukumu zote iko kwake.
 
40Na ikiwa tukikuonyesha baadhi ya tuliyo waahidi au tukakufisha kabla yake, juu yako wewe ni kufikisha ujumbe na juu yetu ni hisabu.
 
41Je! Hawakuona kwamba tunaifikia ardhi tukiipunguza nchani mwake? Na Mwenyezi Mungu huhukumu, na hapana wa kupinga hukumu yake, naye ni Mwepesi wa kuhisabu.
 
42Na walipanga walio kuwa kabla yao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye mipango yote. Yeye anajua inayo chuma kila nafsi. Na makafiri watajua ni ya nani nyumba ya mwisho Akhera!
 
43Na walio kufuru wanasema: Wewe hukutumwa. Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi, na pia yule mwenye ilimu ya Kitabu.