113 - AL - FALAQ |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko, |
|
2 | Na shari ya alivyo viumba, |
|
3 | Na shari ya giza la usiku liingiapo, |
|
4 | Na shari ya wanao pulizia mafundoni, |
|
5 | Na shari ya hasidi anapo husudu. |
|