97 - AL - QADR |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu. |
|
2 | Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri? |
|
3 | Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu. |
|
4 | Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo. |
|
5 | Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri. |
|