92 - AL - LAYL |
|
|
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. |
|
|
1 | Naapa kwa usiku unapo funika! |
|
2 | Na mchana unapo dhihiri! |
|
3 | Na kwa Aliye umba dume na jike! |
|
4 | Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali. |
|
5 | Ama mwenye kutoa na akamchamngu, |
|
6 | Na akaliwafiki lilio jema, |
|
7 | Tutamsahilishia yawe mepesi. |
|
8 | Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake, |
|
9 | Na akakanusha lilio jema, |
|
10 | Tutamsahilishia yawe mazito! |
|
11 | Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia? |
|
12 | Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu. |
|
13 | Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia. |
|
14 | Basi nakuonyeni na Moto unao waka! |
|
15 | Hatauingia ila mwovu kabisa! |
|
16 | Anaye kadhibisha na kupa mgongo. |
|
17 | Na mchamngu ataepushwa nao, |
|
18 | Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa. |
|
19 | Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa. |
|
20 | Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa. |
|
21 | Naye atakuja ridhika! |
|